
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 24, 2014, saa 11: 56 jioni
KIUNGO wa Dar Young Africans, Omega Seme, amesema kwasasa hana muda wa
kupoteza zaidi ya kufanya mazoezi makali ya kujiweka fiti tayari kwa kuitumikia
klabu yake msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajia kuanza kutimua
vumbi mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza na MPENJA
BLOG jioni hii, Omega aliyekuwa anacheza kwa mkopo Tanzania Prisons msimu
uliopita amesema kuwa anafahamu Yanga
kuna viungo bora, lakini imani yake ni kupata namba ya kudumu kutokana na
maandalizi anayoyafanya kwa sasa.
“Kupata namba inategemea na mwalimu. Yeye ndiye
anajua. Cha msingi ni kujiweka fiti, mwalimu akiona ninafaa basi atanipa namba”.
Alisema Omega.
Omega aliongeza kuwa uwepo wa Hassan Dilunga na
Haruna Niyonzima katika nafasi ya kiungo ni changamoto kubwa kwake, lakini hana
wasiwasi kwasababu anajiona mwenye uwezo mkubwa wa kupambana nao.
Kiungo huyo aliwaondoa hofu mashabiki wa Yanga juu
ya kurejea kwake na kuwataka kuwa na subira ili kumuona akiwa katika kiwango
cha hali ya juu.
Kurejeshwa kwa Omega kwa asilimia kubwa kumetokana
na kuondoka kwa kiungo mahiri wa Yanga sc, Frank Domayo aliyejiunga na mabingwa
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc.
Akizungumzia kuongezeka kwa vijana katika timu za
ligi kuu, Omega alisema ni jambo jema na anaomba timu zizidi kuwaamini makinda
kwasababu wana uwezo wa hali ya juu.
“Vijana wapewe nafasi kwasababu wanaweza
kuzisaidia timu zetu na timu ya Taifa”. Alisema Omega.
Kuhusu Taifa stars, Omega alikiri kutamani
kuichezea kwasababu timu hiyo kwasasa ni
nzuri na ina wachezaji wazuri.
“Stars inacheza vizuri. Nikipata nafasi nitafurahi
kuitumikia nchi yangu”.
0 comments:
Post a Comment