
Na
Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 24, 2014, saa 11:00 asubuhi
WASHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samata
na Thomas Emmanuel Ulimwengu kesho jumapili wanatarajia kuiongoza TP Mazembe
katika mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya
wapinzani wao wakubwa, AS Vita mjini Lubumbashi.
Timu
hizi hasimu zitakutana katika mchezo wa kesho zikiwa na kumbukumbu ya
kusababisha maafa ya vifo vya watu zaidi ya 15 katika mchezo wao wa ligi kuu ya
DR Congo wiki za karibuni.
Tukio
hilo baya lilitokea mjini Kinshasa baada ya mashabiki wa AS Vita kutoridhishwa
na kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzania wao TP Mazembe.
Mchezo
wa kesho umevuta hisia za mashabiki wengi wa soka, kwani timu hizi
zinapokutana, upinzani unakuwabmkubwa mno nje ya uwanja na ndani ya uwanja.
TP
Mazembe wataingia katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kupigwa
bao 1-0 kwenye mchezo wao wa kwanza wa
kundi A na Al Hilal ya Sudan mnao mei 17
mwaka huu.

Mei
18 mwaka huu, AS Vita walitumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuilaza
Zamalek ya Misri mabao 2-1, hivyo wataingia katika mchezo huo wa kundi A wakiwa
na morali kubwa ya kusaka ushindi wa pili.
Mechi
nyingine ya kesho jumapili itakuwa ya Kundi B kati ya wenyeji ES Setif ya Algeria dhidi ya SC Sfaxine ya
Tunia.
Mei
18 mwaka huu SC Sfaxine waliifumua Al Ahly Benghazi ya Libya mabao 3-1, wakati
mei 17, 2014, ES Setif waliifunga mabao 2-1 Esperance ya Tunisia.
Mbali
na mechi hizo za kesho, leo hii mitanange mingine inaendelea ambapo kundi A,
wenyeji Zamalek watawakaribisha Al Hilal kutoka nchini Sudan.
Huu
utakuwa mchezo muhimu kwa Mafarao waliopoteza mechi iliyopita. Al Hilal wao
watakuwa wanahitaji ushindi wa pili katika michuano hiyo.
Mechi
ya kundi B leo hii, wenyeji Al Ahly
Benghazi ya Libya waliopoteza mechi ya kwanza kwa mabao 3-1 watakabiliana
na miamba ya soka la Tunisia, Esperance
ambao nao mechi ya kwanza walilala kwa mabao 2-1.
0 comments:
Post a Comment