
Na Baraka Mpenja, Dar e salaam
CHAMA cha soka Mkoani Mbeya, MREFA kimewaomba
mashabiki wa soka mkoani humo kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa
ya Tanzania, Taifa stars katika mchezo
wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Malawi hapo kesho uwanja wa Sokoine.
Katibu mkuu wa MREFA, Seleman Haroub ameueleza
mtandao huu kuwa Mbeya wamepata bahati ya kuiona Taifa stars kwa mara ya kwanza
ikicheza katika ardhi yake, hivyo wasiwaangushe Watanzania wenzao.
“TFF wametuamini na kutuletea pambano hili la
kimataifa. Ni fursa nyingine kwa mashabiki kuwaonesha watanzania kuwa Mbeya
wanapenda Mpira”.
“Wajitokeze kesho kwa wingi kuishangilia Taifa
stars. Kuna mikoa mingi ambapo mechi hii ingechezwa, lakini jitihada za MREFA
kwa kushirikiana na wamiliki wa uwanja wa Sokoine zimeleta mechi hii”.
“Hii ni mechi ya Kimataifa, ujue TFF wameridhishwa
sana na mazingira ya uwanja wa Sokoine kwa sasa, na ndio maana wameamua kuileta
Taifa stars”
“Sasa wana Mbeya tusiwe nyuma ili siku zijazo
tuendelee kupata nafasi kama hii iliyozoeleka kwa mikoa ya Arusha (miaka ya
nyuma), Mwanza na siku zote Dar es salaam”. Alisema Haroub.

Kwa upande wake meneja wa uwanja wa Sokoine,
Modestus Mbande Mwaluka alisema maandalizi ya uwanja yamekamilika kwa asilimia
95.
“Jana tumefanya kazi kubwa ya kumalizia kupata
rangi vyumba vya kisasa vya kubadilishia nguo.”
“TFF waliagiza hilo lifanyike kabla ya mechi.
Tumeshirikiana na wadau na kukamilisha zoezi hilo”
“Unajua Mbeya, watu wanapenda mpira na kama umewahi kufika
kwenye mechi za Mbeya City basi utaamini hilo”.
“TFF wametuamini na wametuletea timu ya Taifa,
nasisi tumejipanga kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri”.
“Uwanja uko tayari na nikiwa meneja malengo yangu
ni kuhakikisha tunapata mechi nyingi za kimataifa”. Alisema Mwaluka.
Kiingilio katika mechi hiyo ya kwanza kwa kocha mpya wa Taifa
stars, Mart Nooij kitakuwa sh. 5,000
wakati tiketi zitauzwa siku ya mchezo kuanzia saa 2 asubuhi katika vituo vya
Uyole, Mwanjelwa,, Mbalizi, Stendi Kuu, Holiday Inn na Uwanja wa Sokoine.
Magari yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani ni ya wachezaji, gari
la wagonjwa, gari la zimamoto na gari la waamuzi pekee.
0 comments:
Post a Comment