
SHIRIKISHO
la soka duniani FIFA, limetupilia mbali maombi ya kiungo wa Porto, Mbrazil,
Fernando kutaka kuichezea timu ya taifa ya Ureno katika fainali za kombe la
dunia mwaka huu nchini Brazil kuanzia juni 12 hadi julai 13.
Kiungo
huyo mzaliwa wa Brazil alipata uraia wa Ureno mwezi desemba 2013, lakini anatakiwa
kuiwakilisha Brazil katika mashindano ya kimataifa na si Ureno.
Baada
ya Ureno kuona FIFA wamemruhusu Mbrazil, Diego Costa kuichezea Hispnia katika
fainali za kombe la dunia mwaka huu, waliona ipo haja na wao kumuombea
Fernando, lakini FIFA wameweka wazi kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 26 hawezi
kuicheza Ureno.
FIFA
wamesema Fernando anaweza kuicheze nchi yake aliyozaliwa kwasababu mwaka 2007
aliiwakilisha Brazil katika kampeni za kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia
kwa vijana chini ya miaka 20.
Taarifa
iliyotolewa na chama cha soka nchini Ureno jana inasema: “Chama cha soka nchini
Ureno kimepokea taarifa leo hii (jana) kutoka FIFA kuwa mchezaji Fernando hawezi
kuiwakilisha timu ya taifa ya Ureno”.
“FIFA
wamesema mchezaji huyu hakuwa na uraia wa Ureno alipokuwa anaichezea Brazil
kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia kwa vijana chini ya miaka 20 kama
inavyotakakiwa na shirikisho”.
Fernando
ambaye amecheza mechi 38 katika mashindano yote msimu huu akiwa na Porto, kwa
muda mrefu amekuwa akihusishwa kujiunga na Machester City inayoshiriki ligi kuu
soka nchini England.
0 comments:
Post a Comment