
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 10:36 jioni
BAADA ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita,
maafande wa Mgambo JKT kutoka jijini Tanga wanatarajia kuanza kambi yao juni 9
mwaka huu tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo, Moka Shaban Dihimba
amezungumza na MPENJA BLOG na kueleza
kuwa malengo ya kuingia kambini mapema ni kukwepa majanga ya msimu uliopita
ambapo waliponea chupuchupu kurudi ligi daraja la kwanza.
“Tutabaki na wachezaji wote. Hatuachi mtu, lakini
tunatarajia kuongeza nguvu hususani safu ya ushambuliaji”. Alibainisha Moka.
“Timu ilivyosajiliwa mara ya kwanza sisi
hatukuwepo. Tulipoingia makocha wapya tulijitahidi kuhakikisha timu haishuki
daraja, lakini kuna nafasi tumeona tunahitaji kurekebisha ili tusifanye vibaya
kama ilivyotokea msimu uliopita”.
Moka aliongeza kuwa wakirudi kambini mwezi ujao, wataalika
wachezaji kutoka sehemu mbalimbali ili kuwafanyia majaribio kama baadhi ya timu
zifanyavyo.
Aidha, alisisitiza kuwa msimu ujao wanahitaji
kuonesha makali kama Mbeya City fc kwasababu mechi za mwishoni mwa msimu walivuna
pointi nyingi na ilidhihirisha kuwa mambo yanawezekana.
‘Katika majaribio ya wachezaji tutazingatia umri.
Hatutahaingaika na wachezaji waliotoswa na timu nyingine.”
“Ukichukua vijana wadogo unaweza kukaa nao misimu
miwili mpaka mitatu. Ukichukua wakongwe unaweza kukaa nao msimu mmoja na wakachoka”.
Alisema Moka.
0 comments:
Post a Comment