
Imechapishwa mei 23, 2014, saa 7:48 mchana.
KIUNGO wa Bayern Munich Toni Kroos hana nia ya kuwa mchezaji wa Manchester United msimu ujao.
Kwa
muda mrefu nyota huyo amekuwa akiwindwa na wakali hao wa Old Trafford
hususani wakati huu ambapo suala lake la mkataba mwingine halijatatuliwa
na Bayern.
Kroos,
24, amebakiwa na mwaka mmoja katika mkataba wake na yuko tayari
kukubali ofa ya kuongezewa mkataba mwingine na sio kuondoka klabuni
hapo.


Kagoma kuondoka: Kroos anayewindwa na Manchester United ataichezea Ujerumani katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Kroos aliyeng`arishwa na kocha mpya wa Manchester United, Louis van Gaal wakati huo akiwa Bayern inasemekana kuwa ana nia ya kufanya kazi na kocha wake huyo wa zamani, lakini amekuwa akikanusha kuwa miamba hiyo ya Uingereza haipo katika rada zake.
Akizungumza na Bild
alisema: 'Natarajia kuichezea Bayern Munich msimu ujao.
"Kuna tetesi nyingi sana, lakini Manchester sio na haitakuwa ishu".
"Kwa muda huu mawazo yote yapo katika maandalizi ya kombe la dunia 2014".
Man United wakati huo wakiwa chini ya David Moyes walikubaliana na Bayern kulipa ada ya uhamisho ya paundi milioni 20 ili kuinasa saini ya Kroos.
Wakati huo huo, rais wa Bayern, Karl Hopfner, anadai Kroos atapewa ofa nzuri ya mkataba mpya kutoka klabu ya Bayern Munich.

0 comments:
Post a Comment