Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 5:46 usiku
TAARIFA zilizoifikia MPENJA BLOG kutoka mjini Khartoum nchini Sudan usiku huu ni kwamba
wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc
chini ya kocha mkuu Juma Mwambusi wamefungwa mabao 2-1 na AFC Leopard ya Kenya katika
mchezo uliopigwa kuanzia majira ya saa 2:00 kamili usiku mjini Khartoum.
Bao la Mbeya City fc limefungwa na kiungo
mshambuliaji, Deus Kaseke.
Hata hivyo inaelezwa kuwa mchezo huo ulikuwa mzuri
kwa timu zote, lakini AFC walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza.
Ushindi huo unawafanya AFC Leopard wakae kileleni
mwa kundi B baada ya kufikisha pointi 6.
Endelea kufuatilia mtandao huu, utakupatia habari
kamali hivi punde.
0 comments:
Post a Comment