![]() |
Hans Poppe hamtaki kabisa Richard Wambura |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 1:44 usiku
MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi ya Simba
unaotarajia kufanyika juni 29 mwaka huu, mwanasheria na wakala wa wachezaji wa
FIFA, Dkt. Damas Daniel Ndumbaro anatarajia kuanika hatima ya majina ya
wagombea wote waliowekewa pingamizi.
Wana Simba wengi wanasubiri kwa hamu kusikia hatima
ya wagombea wa nafasi mbalimbali waliowekwa kitanzini na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo kwasababu
tofauti tofauti.
Mgombea Urais, Michael Richard Wambura ni moja ya
wagombea wa Urais aliyewekewa pingamizi, hivyo wafuasi wake waliomsindikiza kwa
mbwembwe nyingi wakati wa kuchua na kurudisha fomu wanasubiri kwa hamu hatima yake.
Kamati ya uchaguzi jana imefanya kazi ya kuwasikiliza
watu walioweka mapingamizi na wagombea waliowekewa pingamizi.
Awali Ndumbaro alisema kamati yake haitamuengua
mgombea yeyote isipokuwa kanuni za uchaguzi za TFF na katiba ya Simba ndio
itamuengua mgombea.
Ndumbaro alisema kamati yake itawaondoa wale wote
walioenda kinyume na kanuni za uchaguzi na kusisitiza kuwa kamati yake ina watu
makini na haitathubutu kupindisha sheria.
Wakati hayo yakijiri, Michael Richard Wambura amewasilisha
malalamiko yake kwa kamati ya uchaguzi akisema baadhi ya watu wamekiuka kanuni
za uchaguzi kwa kuwapigia kampeni baadhi ya wagombea kabla ya muda uliotajwa.
![]() |
Richard Wambura anapambana na Hans Poppe, Ndumbaro ndiye mwenye maamuzi |
“Nimepata ushahidi wa CD ya Hans Poppe akiwaombea
kura Aveva na Kaburu. Pia amasema mimi niliwahi kuiba hela Simba. Nimekabidhi
CD kwa Ndumbaro kwa hatua zaidi na aeleze niliiba wapi hela hizo”. Alisema
Wambura, moja ya wagombe wa Urais.
“Pia nitapeleka CD katika kamati ya maadili ya
TFF. Mtu hawezi kutukana bila sababu”.
“Poppe anasema wasipochaguliwa Kaburu na Aveva
ataacha kuisaidia Simba. Anasema ataondoka katika uongozi. Hii ni nini sasa
kama sio kwenda kinyume na taratibu”.Alikaririwa Wambura.
Mwishoni mwa wiki, mwenyekiti wa kamati ya usajili
ya Simba sc, Keptein Zacharia Hans Poppe alizungumza na mtandao huu na kuweka
wazi msimamo wake kuwa endapo Aveva na kaburu hawatachaguliwa katika uchaguzi
wa Juni 29 atabwaga manyanga.
Poppe alisema amechoka kutoa fedha zake bila
mafanikio yoyote, hivyo anahitaji timu ya uongozi ya Aveva na Kaburu kwani
wanaweza kufanya kazi vizuri.
Mwanajeshi huyo wa zamani wa JTWTZ alibainisha
kuwa Wambura hana uwezo wa kuiongoza Simba kwani wakati wake wa uongozi hakuna
alichokifanya.
Pia alimponda Jamhuri Kiwhelo `Julio` kuwa
hajawahi kufanya lolote akiwa Simba kwani yeye alikuwa kocha na alikuwa
analipwa mshahara, wakati Kaburu
aliyejitahidi kusuka Simba B wakati wa uongozi wake na kuzalisha wachezaji
mahiri wakiwemo Ramadhan Singamo `Messi`, Harun Chanongo, Said Ndemla na
wengineo, hivyo anafaa kuwa makamu wa rais.
0 comments:
Post a Comment