
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 28, 2014, saa 8:55
MAAFANDE wa Polisi kutoka visiwani Zanzibar jana wameondolewa
katika michuano mipya Ya CECAFA Nile Basin Cup baada ya kufungwa mabao 3-0
dhidi ya Victoria Universty ya Uganda .
Huo ulikuwa mchezo wa tatu kwa Polisi kupoteza na
wemeondolewa kwa kufungwa mabao 9 katika mechi tatu bila kufunga hata goli moja.
Walipoteza michezo miwili iliyopita kwa kufungwa idadi ya mabao kama ya
jana dhidi ya Malakia FC na Al Merreikh.
Katika mchezo mwinge hapo jana, Malakia walifungwa
mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Al Merreikh.

Michuano hiyo inatarajia kuendelea leo jioni na usiku
ambapo majira ya saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika mashariki, wawakilishi wa
Tanzania bara, Mbeya City fc watakuwa wanaisaka nafasi ya kucheza robo fainali
ya michuano hiyo kwa kukabiliana na Etincelles mjini Khartoum.
Mbeya City walioanza michuano hiyo kwa kuibuka na
ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Academie ya Burundi na mechi ya pili kufungwa
mabao 2-1 na AFC Leopard, wanahitaji ushindi kwa namna yoyote ile ili kufuzu
hatua ya robo fainali.
Baadaye usiku majira ya 2:00 usiku, AFC Leopard
watakabiliana na ACademie Tchite.
Mjini Sandi, wenye Al –Shandi watakuwa kibaruani
dhidi ya Defence ya Ethiopia.
0 comments:
Post a Comment