Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akimfua bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi |
Imechapishwa Mei 28,2014, saa 9:07
BONDIA
namba moja katika uzito wa light welterweight , Ibrahimu Class 'King
class Mawe' ameibuka na kukemea vikali tabia ya mabondia kwenda
kuangalia ngumi kama wanakwenda kwenye starehe 'Picnic'
Aliyazungumza
hayo katika ukurasa wake wa facebook mapema hivi karibuni akipinga
matukio yanayofanywa na mabondia wakubwa nchini tanzania kwa kuingia
ukumbini huku wakiwa wanakunywa pombe na kushika chupa mbilimbili
Bondia
huyo alienda mbali zaidi kwa kuwaeleza kuwa bondia anapokwenda kwenye
ngumi yupo kazini kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine. hivyo haijalishi
anacheza au hachezi kwa siku hiyo, lazima awe na nidhamu kwa mashabiki
ili upate wapenzi wapya zaidi, kwani wapenzi wa ngumi wanapatikana
kwenye ngumi.


Class
aliongea hayo hivi karibuni baada ya mabondia Mada Maugo na Thomasi
Mashali kuamua kuzipiga kavu kavu kwa kitu kilichotambulika kuwa wao ni
walevi tena wakiwa katika ukumbi wa ngumi Friends Corner Manzese
kitendo hiki cha kupigana hovyo sikiungi mkono hata siku moja kwasababu kinawakosesha thamani mabondia chipukizi.
0 comments:
Post a Comment