


Mwenyekiti wa Spurs , Daniel Levy ameamua kumpatia mkataba wa miaka mitano kocha kijana

Pochettino anasifiwa kwa soka lake la kushambulia katika klabu ya Southampton


Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 3:38 usiku
KLABU ya Tottenham imethibitisha kumteua Mauricio Pochettino kuwa kocha mkuu.
Kocha huyo raia wa Argentina alijiuzulu kuifundisha klabu ya Suthampton baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu soka nchini England , ambapo alisifiwa kuifanya timu hiyo kucheza soka safi la kushambulia.
Pochettino amepewa mkataba wa miaka mitano White Hart Lane na mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, akimrithi kocha aliyetimuliwa, Tim Sherwood.
0 comments:
Post a Comment