
Na Baraka
Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 26, 2014, saa 2:00 usiku
TIMU ya Taifa
ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Malawi katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki uliopigwa jioni ya leo Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Bao pekee la
Stars limefungwa na kiungo mahiri, Amri Ramadhan Kiemba katika dakika ya 35
akimalizia kazi nzuri ya Shomary Kapombe.
Leo hii kocha
wa timu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart
Nooij hakuanzisha kikosi chake kinachojulikana kuwa cha kwanza kwa lengo la
kujaribu wachezaji wanaoweza kumsaidia katika mchezo wa marudiano dhidi ya
Zimbabwe mjini Harare.
Kama
ilivyokawaida, Nooij alimuanzisha mlinda mlango Deogratius Munish `Dida`, Himid
Mao, Edward Charles, Said Mourad, Joram Mgezeke, Shomary Kapombe, Simon Msuva,
Erasto Nyoni, Kevin Friday, Amri Kiemba na Khamis Mcha `Vialli`.
Katika kipindi
hicho, Stars haikucheza vizuri sana tofauti na wapinzani wao Malawi ambao
unaweza kusema walikosa bahati ya kufunga.
Kipindi cha
pili, Nooij alibadilisha karibu kikosi chote ambapo wachezaji kama Kevin
Yondan, Ramadhan Singano, Frank Domayo, Said Juma, Mwinyi Kazimoto.
Ushindi wa leo
unatoa taswira nzuri kwa Stars kuelekea Harare ambapo wanaenda wakiwa na
kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam
Stars
wanaotarajia kuondoka ijumaa mei 30 mwaka huu kwa mujibu wa taarifa kutoka TFF, wanahitaji
ushindi sare ya aina yoyote au ushindi ili kwenda sehemu inayofuata.
Aidha Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura Mgoyo amesema wameandikia TP Mazembe wakiomba kuwapata wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na kabla ya ijumaa wanatarajia kupata majibu.
Aidha Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura Mgoyo amesema wameandikia TP Mazembe wakiomba kuwapata wachezaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu na kabla ya ijumaa wanatarajia kupata majibu.
0 comments:
Post a Comment