
Ofa ya mwisho: Liverpool wameripotiwa kuweka ofa ya paundi milioni 25 kumnasa kiungo wa kimataifa wa England na Southampton, Adam Lallana

Jaribio la pili: Wekundu wa Anfield awali waliweka ofa ya paundi milioni 20, lakini walipigwa chini na Southampto.
Imechapishwa Mei 31, 2014, saa 9:51 asubuhi
LIVERPOOL wameboresha ofa ya kumnasa kiungo wa Southampton, Adam Lallana na kufikia paundi milioni 25.
Wakati huu mchezaji mwenzake Rickie Lambert akitarajiwa kupimwa afya yake kwa lengo la kujiunga na wakali hao wa Merseyside kwa dau la paundi milioni 4, inafahamika kuwa kocha Brendan Rodgers ameamua kuongeza `mkwanja` ili kuinasa saini ya Lallana.
Awali
Wekundu hao wa Anfield waliweka mezani ofa ya paundi milioni 20 na
kukataliwa, lakini wamerudi tena Southampton wakiwa wameongeza dau.
0 comments:
Post a Comment