
Na Baraka Mbolembole
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 12:45 asubuhi
Neno ' Kujiuzulu' lina maana mbili. Ni kuacha, au
kuachia, kazi, haki, madai, au mali. Ni kuacha kufanya jambo, kuachia au
kuachana na kusalimu amri, kukata tamaa; kusema kuwa mtu hatibiki au tatizo
Fulani linakushinda kutatua. Ni kutoa kwa...., au kumuachia mwingine mwenye uwezo
au mamlaka, hasa kwa kudaiwa au kulazimishwa. Kujiuzulu, ni kusalimu amri ya adui
ya kujitolea. Maelezo haya ndiyo maana ya kwanza ya neon Kujiuzulu.
Maana ya pili, Ni kuwa tayari kukubali na kustahimili;
kukubali kuwa jambo Fulani ni lazima liwe, halizuiliki. Ni kukubali kuwa umeshindwa
au utashindwa, na kuwa tayari kustahimili matokeo ya kushindwa. Kujiuzulu, ni kukubali
kusalimu amri ya adui au mpinzani wako na kuwa tayari kustahimili matokeo yake.
Ni kukubali kutekwa, na kuwa tayari kustahimili matokeo ya kuwa mateka.
Kujiuzulu ni kukubali kushindw. Kujiuzulu ni kukubali kustahimili matokeo ya kukata
tamaa na kushindwa jambo!.
Wakati anachuku fomu kasha kurudisha, Michael
Wambura alikuwa mwanachama halali wa klabu ya Simba SC. Kama sivyo hakupaswa kupewa
fomu za kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo unaotaraji kufanyika,
juni 29. Wambura anafahamu kuwa wanachama wa Simba wanataka mabadiliko,
wanahitaji mapinduzi ya kweli, na mapinduzi hayo yatawezeka na kama wanachama wenyewe
wa klabu watasimama kwa umoja katika kuhitaji mabadiliko hayo. Kama mtu atatumia
silaha ambayo haitoi nafasi ya kurudisha nyuma maendeleo anaweza kuibomoa '
ngome ' ya wapinga mapinduzi.
Sababu zote zilizotolewa ambazo zimemfanya,
Wambura ' kuchinjiwa bahari' na kamati ya uchaguzi ya klabu hiyo chini ya wakili,
Damas Ndumbaro, zinaweza kuwa na mashiko ila haziwezi kuficha udhaifu mkubwa uliopo
katika kamati mbalimbali zinazokuwa na dhamana ya kusimamia chaguzi mbalimbali katika
taasisi za soka. Naamini, Wambura aliingia mwenyewe katika uchaguzi huku akifahamu
vita iliyokuwa mbele yake ilikuwa ikionesha ushindi kwa wapinzani wake ambao wanashindwa
kukubali ' msamaha aliouomba' kutokana na kitendo chake cha kuipeleka klabu hiyo
mahakani, mwaka 2010.
Kuna baadhi ya kikundi cha wanachama wa klabu hiyo
kinaamini kuwa ndiyo wenye nguvu na mamlaka na wajuzi wa mambo, lakini sivyo,
atawashinda tu siku moja kwa kuwa yupo mbele yao. Hata kama Wambura anachukiwa,
lakini itabidi wakubali ukweli kwamba ' Wambura ana thamani ya uongozi', ni mtu
makini, hodari na watu wanampenda. Ukitazama safu ya wagombea wa nafasi ya urais
katika uchaguzi ujao wa klabu hiyo, Wambura ndiye mwenye uwezo. Amekata rufaa kupinga
uamuzi huo wa kamati ya uchaguzi.
Simba haihitaji busara
yake? Simba haihitaji juhudi yake ya kufanya kazi na uwezo wake wa kupata matokeo
?.Simba imekuwa ikiongozwa na ' wanakamati hodari' na si viongozi hodari. Simba
imekamatwa na kikundi cha wafanyabiashara wabaya, na wenye nia ya kujikuza.
Wakati, Jamal Malinzi alipoingia, TFF, rais huyo wa soka nchini alitangaza msamaha
kwa wanasoka wote waliokuwa na adhabu za kawaida je, yeye hahusiki katika msahama
huo?
Wambura inawezekana akawa mwanachama halali wa klabu,
ama sivyo kama ilivyotangazwa na kamati ya uchaguzi, ila hawawezi kuficha udhaifu
wao wa kushindwa kuthibitisha baadhi ya saini zilizopo katika nyaraka muhimu.
Kama mtu anasema hajaweka saini, na ikaonekana saini yake. Hapo kuna tatizo na inawezekana
kamati ya uchaguzi iliamua kukimbia na muda bila kufuatilia kwa umakini...
Kamati hii ambayo inaongozwa na mwanasheria maarufu imekosa umakini, imeshindwa
kujiamini, lakini mwisho wa siku imethibitika kuwa, Wambura ni mwanachama anayekubalika
ndani ya klabu hivyo wanachama wengine wanaogombea uongozi wanatakiwa kupambana
naye katika misingi ya demokrasia na sichuki binafsi.
Hawajiamini? Ndiyo, jibu lipo wazi tu, ila ukweli wanachama
wa klabu wanahitaji kumuona katika orodha ya wagombea. Kujiuzulu, si muhimu ila
kamati ya uchaguzi ya Simba inapaswa kusarenda kwakuwa imeshindwa kazi.
Walimpaje fomu za kuwania nafasi muhimu kama si mwanachama?.Huyu mtu ana thamani
ya uongozi, wanachama wa klabu ndiyo wenye kuamua kiongozi wamtakaye
0714 08 43 08
0 comments:
Post a Comment