
Na Baraka Mbolembole
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 12: 53 asubuhi
Timu ya soka ya Taifa ya Australia, maarufu kama '
Soccerrose' ndiyo timu inayoshikilia rekodi ya kufunga magoli mengi katika mchezo
mmoja duniani. Australia waliichapa, American Samoa magoli 31-0, April 11, 2001 katika mchezo wa kimataifa
unaotambuli wa na FIFA...Soccerrose, walitua nchini, Brazil siku ya jana tayari
kwa michuano ya kombe la dunia inayotaraji kuanza kutimua vumbi, juni 12.
Australia ipo katika kundi la pili sambamba na mabingwa watetezi, Hispania,
makamu bingwa wa fainali zilizopita, Uholanzi, na Chile.
Kikosi cha kocha, Ange Postecoglou kimeshawahi kucheza
michuano hiyo mara tatu na mafanikio yao makubwa ni kufika hatua ya 16 bora,
mwaka 2006... Kwa mara ya kwanza, Australia, ilifuzu kwa fainali za mwaka 1974
zilizofanyika nchini Ujerumani na kuondoka patupu. Walipata suluhu-tasa dhidi ya
Chile, kisha wakapoteza kwa waliokuwa wenyeji wa michuano, Ujerumani Mashariki,
na Ujerumani Magharibi na kuondoshwa mashindanoni pasipo kufunga goli lotote.
Ikiwategemea zaidi wachezaji wake wazoefu kama Tim Cahiil, na nahodha wa kikosi
hicho, Michael Jadinak ambaye anakipiga katika kikosi cha Crystal Palece ya England
,kikosi hicho kimekuwa timu ya kwanza kuwasili, Brazil.
Timu hiyo haina rekodi ya kutisha katika michuano ila
katika fainali mbili za mwisho wameonekana kupata uzoefu wa michuano na watamtegemea
zaidi mfungaji wao bora wa muda wote, Cahill kuongoza safu ya mbele, kiungo huyo
mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Everton ameifungia nchi yake jumla ya magoli
31 katika michezo 67, huku magoli matatu akiwa amefunga katika kombe la dunia.
Cahill mfungaji wa goli la kwanza la Soccerrose,
katika michuano hiyo hucheza kwa nguvu na kushambulia moja kwa moja, pia ni mtaalamu
wa kucheza mipira ya juu, kwasasa hucheza zaidi katika nafasi na mashambulizi,
japo wakati mwingine hucheza kama kiungo wa kati, kiungo wa mashambulizi au
mshambuliaji wa pili. Tim, alifunga magoli matatu katika fainali za Ujerumani wakati,
nchi yake ilipoichapa, Japan katika mchezo wa kwanza katika kundi ambalo walipangwa
pamoja na Brazil, Japan na Croatia. Chini ya kocha, Mdachi, Guus Hiddink timu hiyo
ilifanikiwa kuvuka kundi hilo.
Ilifungwa na Brazil katika mchezo wa pili, kabla ya
kulazimisha sare ya kufungana magoli 2-2 na Croatia. Katika hali ya utata walitolewa
na Italia katika hatua ya 16 baada ya kulala kwa goli 1-0 ndani ya dakika 120.
Walirudi tena katika fainali za miaka minne iliyopita nchini, Afrika na kuishia
hatua ya makundi. Walichapwa magoli 4-0 na Ujerumani katika mchezo wa kwanza,
wakalazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Ghana, na kuifunga, Serbia magoli 2-1
katika mchezo wa mwisho.
Tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ilifanya mabingwa
hao mara nne wa zamani wa bara la Asia, kurudi nyumbani kwani, Ghana waliungana
na Ujerumani kufuzu kwa hatua ya pili baada ya kuwa na wastani mzuri wa magoli.
Je, watafanya nini nchini, Brazil katika fainali zao za nne kushiriki. Wataanza
kwa kucheza na Chile, juni 13, kasha watacheza na Uholanzi, juni 18, na kumaliza
michezo yao ya makundi kwa kuwakabili, Hispania, juni 23. Staili yao ya uchezaji
si ya kuzuia, ila ni timu ngumu kuifunga kama wapinzani.
0 comments:
Post a Comment