
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 10: 48 jioni.
KIUNGO mahiri aliyeichezea Simba sc msimu
uliopita, Henry Joseph Shindika amesema bado hajazungumza na timu yoyote mpaka
sasa kueleka msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Joseph aliyemaliza mkataba na Simba mwishoni mwa
msimu uliopita ameiambia MPENJA BLOG
kuwa nia yake ni kuendelea kucheza ligi ya Tanzania msimu ujao, lakini hajui
ataitumikia klabu gani.
“Kwasasa sijapata mchakato wowote, lakini kuna
mambo nayaweka sawa, muda si mrefu nitawajulisha mashabiki wangu”. Alisema
Joseph.
Kuhusu kucheza soka la kulipwa kwa mara nyingine,
Joseph alisema bado hajapata timu yoyote, lakini kama itatokea nafasi ataondoka
zake kusaka maisha mapya.
“Sijajua nitacheza wapi, mpira kazi yangu. Kokote
kule nitaenda. Ikitokea nafasi nje nitaelekea huko”. Aliongeza Joseph.
Usajili wa majira ya kiangazi kueleka msimu wa
2014/2015 wa ligi kuu soka Tanzania bara unatarajia kufunguliwa rasmi juni 15
mwaka huu, lakini baadhi ya klabu kama Azam fc tayari zilishanasa majembe
mapya.
Mabingwa hao wa ligi kuu soka Tanzania bara walishasajili
wachezaji wawili kutoka Yanga, Frank Domayo `Chumvi` na Didier Kavumbagu.
Nao Yanga walishamuongezea mkataba beki wao kisiki,
Mbuyu Twite aliyekuwepo katika rada za Azam fc.
Aidha, Joseph aliwatakia kila la heri Taifa stars
kuelekea katika mchezo wa marudiano juni 1 mwaka huu mjini Harare dhidi ya
wenyeji Zimbabwe.
“Kikubwa wachezaji wajitume tu. Wasijaribu
kuwadharau Zimbabwe kwasababu lolote linaweza kutokea ugenini”. Alishauri
Joseph.
0 comments:
Post a Comment