
Imechapishwa Mei 23, 2014, saa 11: 10 jioni
Golikipa wa zamani wa timu ya soka ya Simba, Juma Kaseja, 29 katikati ya mwanzoni mwa wiki hii alikuwa mmoja wa watu watatu kati ya 34 waliohitimu mafunzo ya ukocha daraja A. Kaseja ambaye anaichezea timu ya Yanga kwa sasa, alianza kucheza ligi kuu Tanzania Bara, mwaka 2001 katika timu ya Moro United akiwa na miaka 17, amecheza katika klabu tatu tofauti nchini katika muda wa miaka 13 sasa. Ni mafanikio ambaye yatamfanya kuwa tayari kwa kazi ya ukocha miaka ya mbele. Mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo, Kaseja alisema bado ataendelea kucheza soka huku akitumia kozi hiyo ya mafunzo ya ukocha kujihimarisha zaidi kiuchezaji kwa kuwa ameweza kufahamu mambo mengi ya kiufundi ambayo awali hakuwa akiyafahamu vizuri au kuyajua kabisa.
Kuna wachezaji wachache sana ambao wamefikia
mafanikio yake ya kiuchezaji. Akiwa mshindi wa mataji saba ya ligi kuu Tanzania
Bara, huku akiwa na tuzo nyingi binafsi, Kaseja anafuata mkumbo wa wachezaji
wengi wa soka barani Ulaya ambao waliingia katika mafunzo ya ukocha wakiwa
badowachezaji. Wiki hii klabu ya FC Barcelona, ilitangaza kumpatia majukumu ya
ukocha mchezaji wao wa zamani, Luis Enlique, Manchester United itaongozwa na
mchezaji wake wa zamani, Ryan Giggs ambaye ameamua kustaafu kucheza soka la
ushindani, Claude Makelele ameachia kazi ya usaidizi chini ya Laurent Blanc
katika klabu ya PSG na kuanzia msimu ujao atakuwa kocha wa timu ya Bastia
ambayo pia inacheza katika ligi kuu ya Ufaransa, Lieague 1.

Willy
Sagnol mlinzi wa zamani wa Ufaransa na klabu ya Bayern Munich anataraji kuwa
kocha mkuu wa mabingwa wa zamani wa Liegue 1, klabu ya Bordeaux. Si hao tu,
tumeshaona mafanikio ya makocha kama, Pep Guardiola, Carlo Ancelotti, Gustavo
Poyet, Diego Simeone na wengineo ambao waliingia katika kazi ya ukocha na
kufanikiwa muda mfupi baada ya kustaafu soka. Ukitoa, Kaseja, kwa upande wa
Tanzania wapo wachezaji wengi wa zamani ambao walijitumbukiza katika kazi ya
ukocha lakini hakuna ambaye ameweza kupata mafanikio yanayoonekana. Si kwamba
hawana uwezo, hapana, bado watawala wa soka Kwa nini wachezaji wa zamani wa
Tanzania wanashindwa kufikia mafanikio hayo?
Mtazame kocha Juma Mwambusi, Mwalimu huyo amekuwa
akionesha uwezo mkubwa wa ufundishaji katika miaka ya karibuni . Mwaka 2008, aliisaidia klabu
ya Tanzania Prisons ya Mbeya kumaliza
katika nafasi ya pili katika ligi kuu
Tanzania Bara, na msimu uliomalizika aliweza kuisaidia timu iliyokuwa ikicheza ligi kuu kwa mara ya
kwanza kumaliza katika nafasi ya tatu. Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha timu
ya Polisi Dodoma na kushuka daraja chini
yake, aliipandisha daraja Mbeya City na kufanya mambo makubwa ila bado hakuna
uwezekano way eye kufundisha klabu kubwa za Tanzania kwa kuwa timu hizo
zimewekeza mawazo yao kwa Walimu wa kigeni.
Kwa sasa Tanzania imekuwa ikiweka mkakati wa
kuinua soka la ndani, ila mkakati huo
ni lazima uendane na maboresho ya miondo mbinu, viwanja, timu za watoto na
kuwaendeleza makocha wazawa kwa kuwapatia kozi zaidi ambazo zitawaongezea ujuzi
wa ufundishaji. Si kila mchezaji mahiri anaweza kuwa kocha bora ila ukitoa ,
makocha kama Charles Boniface Mkwasa, na
Abdallah Kibadeni, makocha wengine wakiongozwa na Jamhuri Kiwelo na Fred
Minziro japokuwa walicheza kwa mafanikio
katika klabu za Simba na Yanga, na kuonesha uwezo wao wa ufundishaji wakiwa
katika klabu ndogo wameishia kuwa makocha wasaidizi na si rahisi kwao kuwa
makocha wakuuu katika klabu hizo. Kwa nini?
![JUMA_KASEJA[1]](http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/JUMA_KASEJA1-680x1024.jpg)
Mfumo wa ufanyaji kazi kwa mazoea kutoka kwa
viongozi wengi wa soka nchini umepelekea wachezaji wengi wa zamani kushindwa
kupata mafanikio katika kazi ya ukocha . Wapo wanaosema kuwa mapenzi ya u-Simba
na u-Yanga yamefanya wapenzi wengi kukosa imani na makocha wazawa kupewa kazi
hiyo, Simba ama Yanga na badala yake wamekuwa wakirubuniwa kutoka timu ndogo
kila wanapofanya vizuri na kupewa kazi ya usaidizi katika timu hizo
wanazozifahamu vyema. Hili ni kosa, ni lazima tuwapromoti makocha wetu wazawa
ili siku moja waweze kusaidia mpira wa Tanzania kwa kuzalisha wachezaji wengi
vijana.
Mecky Mexime
ameichezea Mtibwa kwa maisha yake yote ya soka la ushindani, na sasa
akiwa na miaka miwili katika kazi ya ukocha wa timu hiyo, Mecky anatakiwa
kupandisha kiwango chake cha ufundishaji ili kujiweka katika orodha ya makocha
ambao Tanzania inaspaswa kujivunia. Mecky angweza kuwa kama Gary Neville ambaye
mara baada ya kustaafu soka la ushindani, Roy Hodgson alimchukua Neville na
kumfanya msaidizi wake katika timu ya England jambo ambalo kwetu sisi si rahisi
kutokea kwa kuwa ni wachezaji wachache ambao wamekuwa wakifanya jitihada za
kweli za kuwa makocha bora.
Kwa nini, Suleiman Matola anakuwa kocha msaidizi
katika timu ya Simba hadi hivi leo?. Matola amechezea Simba kwa mafanikio
makubwa, zaidi tangu alipojiingiza katika kazi ya ukocha ameonesha kitu kikubwa
anacho. Matola ni mshindi kiuchezaji na kiufundishaji. Ameshinda mataji kadhaa
ya Uhai Cup akiwa kocha wa kikosi cha pili, aliwahi kushinda ubingwa wa kombe
la Taifa Cup akiwa kocha wa Mkoa wa Singida na zaidi ndiye ambaye amewezesha
timu ya Simba kuwa na vijana bora ambao kwa miaka miwili ya ukata klabuni hapo
chipukizi hao wameweza kuziba virika Simba. Huyu ana uwezo mkubwa wa
kiufundishaji lakini mbona bado makocha wetu wazawa hawapandishwi na kuwa
makocha wakuu katika klabu kubwa?
UKitoa udhaifu wetu wa kuhitaji mambo makubwa na
sifa , makocha wenyewe wanaweza kujifunza zaidi na kupandisha viwango vyao
ambavyo vinaweza kuzivutia timu za jje ya nchi na wakaenda huko kupata uzoefu wa kiufundishaji. Mbona kina,
Tom Olaba , Sam Timbe, James Siang’a, Moses Basena na wengine wanatoka nchi za
Kenya na Uganda na kuja Tanzania kuzifundisha timu zetu kubwa? Hongera, Juma
Kaseja kwa kujiandalia mazingira ya kazi mpya siku za mbeleni. Kutoka uchezaji,
hadi ufundishaji, Juma Kaseja anaweza kuwa kocha mzuri katika miaka ijayo kama
tutajifunza kutokana na makosa yetu.
0713 08 43 08
0 comments:
Post a Comment