Na Baraka Mpenja
Imechapishwa Mei 24, 2014, saa 1:30 usiku
UNAKUMBUKA ule moto wa Mbeya City katika michuano
ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita?.
Wawakilishi hao wa Tanzania wamehamishia kasi yao
katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup, ambapo wameanza vyema
mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Academie Tchite
ya Burundi.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na washambuliaji
hatari Paul Nonga katika dakika ya 15,
Mwegane Yeya dakika ya 27 na nyota mpya Them Felix katika dakika ya 37.
Mechi hiyo muhimu kwa Mbeya City fc iliyosuasua
kuwasili Sudan kutokana na kucheleweshewa tiketi za ndege imepigwa katika
uwanja wa Khartoum-Sudan.
Kikosi cha Mbeya City kilichoanza leo ni Barhan David,
Kabanda John, Kibopile Hamad, Julius Deogratius, Yohana Morris, Antony
Matogolo, Deus Kaseke, Mazanda Steven, Paul Nonga, Mwegane Yeya na Them Felix
`Mnyama`.
Mbali na mchezo wa Mbeya City fc, majira ya saa 2:00 usiku AFC Leopard ya Kenya itakabiliana na Enticelles ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment