Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
HATIMAYE safari ya Mbeya City fc kwenda kushiriki
michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup nchini Sudan imekamilika baada ya kutumiwa
tiketi za ndege.
Kocha msaidizi wa klabu hiyo Maka Mwalyisyi
amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita na kueleza kuwa wamepokea
tiketi na wanaanza safari alfajiri ya kuamkia kesho na wanatarajia kufika Sudan
kesho ijumaa majira ya saa 11:00 asubuhi
kwa saa za huko.
Mwalwisyi amesema kwa mujibu wa Ratiba wanatakiwa
kushuka dimbani kesho dhidi ya El Mereikh ya Sudan, lakini wapo katika
mazungumzo ya kuomba kubadilishiwa ratiba kwasababu watakuwa wamechoka na
safari.
“Tulitakiwa kucheza kesho. Lakini kuna mazungumzo
yanaendelea ili kubadilishia ratiba. Kila kitu kinakwenda sawa na muda si mrefu
tutaeleza kitakachojiri”. Amesema Mwalwisyi.
Hata hivyo, Mwalwisyi amesema wachezaji wote wapo
katika hali nzuri na wamefurahi kuona safari imekamilika.
Mwalwisyi amesema kwa muda wote waliokuwepo Dar es
salaam walikuwa wakifanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Licha ya kuchelewa kuondoka nchini, kocha huyo
amesema sio kigezo cha kushindwa kufanya vizuri.

0 comments:
Post a Comment