![]() |
Kocha bora wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, Juma Mwambusi (kulia) |
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Mei 30, 2014, saa 7:05 mchana
ROBO fainali ya michuano ya CECAFA Nile Basin Cup
inayoendelea kushika kasi nchini Sudan inatarajia kuanza kuunguruma leo jioni mjini
Khartoum kwa mechi mbili kupigwa katika uwanja wa Merreikh.
AFC Leopard waliomaliza wa kwanza katika kundi B
kwa kukusanya pointi 9 (ushindi wa asilimia 100) watakabiliana na Defence ya
Ethiopia majira ya saa 12:30 jioni kwa
saa za Sudan.
Usiku saa 2:30, wenyeji Al-Merreikh walioshika
nafasi ya kwanza kundi A Kwa kujikusanyia
pointi 7 watakuwa na kibarua cha kufa mtu dhidi ya Academie Tchite ya Burundi.
Robo fainali za pili zitaendelea kesho jumamosi (Mei 31) ambapo
mechi ya kwanza itakayoanza saa 11:30 jioni itakuwa baina ya wagonga nyundo wa
Mbeya, Mbeya City fc dhidi ya Victoria University ya Uganda. 

Wawakilishi hao wa Tanzania walimaliza hatua ya
makundi kwa kushika nafasi ya pili kundi B baada ya kujikusanyia pointi 4
katika michezo mitatu.
Mbeya City walianza kampeni zao kwa kuwafunga
Academie Tchite mabao 3-2, mechi ya pili wakalala kwa mabao 2-1 dhidi ya AFC
Leopard na mechi ya mwisho walitoka suluhu na Entincelles.
Ushindi katika mechi hiyo ni muhimu kwa kocha Juma
Mwambusi kwani kucheza nusu fainali itakuwa historia nzuri ikizingatiwa ni mara
yao ya kwanza kucheza michuano mikubwa ya kimataifa.
Hata kama walishiriki mapinduzi Cup mwanzoni mwa mwaka
huu visiwani Zanzibar na kukutana na timu za nje ya nchi, michuano ya Nile
Basin Cup inashirikisha timu nyingi za kigeni.
Kwa maana hiyo, Mbeya City wanahitaji ushindi ili
kuwafurahisha watanzania wanaowaombea dua kila kukicha.
Mechi ya pili itaanza majira ya saa 2:00 usiku kwa kuwakutanisha Al-Shandi dhidi ya
Malakia FC.
0 comments:
Post a Comment