Na
Baraka Mpenja , Dar es salaam
0712461976
KIPIGO
walichokipata Yanga sc kutoka kwa Mgambo JKT machi 30 mwaka huu kwenye uwanja
wa CCM Mkwakwani, jijini Tanga kimezidi kuwavuruga zaidi viongozi, makocha, na
mashabiki wa klabu hiyo.
Imeonekana
kuwa ajabu kwa Mgambo JKT kuwafunga Yanga, wakati mpira wa miguu huwa una
matokeo ya aina hiyo.
Katika
mechi, wachezaji 22 wanapambana kwa maana ya wachezaji 11 kwa kila timu.
Kama
wachezaji wanakuwa sawa kwa timu zote kwa mujibu wa sheria, basi kushinda ni
haki kwa timu yoyote.
Lakini
kuna wakati timu moja inaweza kujipa matumaini zaidi ya kushinda mechi na
kusahau kuwa inaenda kucheza na watu waliojiandaa kama wao.
Hakuna
ubishi, kupata matokeo kunatokana na mipango mizuri ya uwanjani na nje ya
uwanja.
Viongozi
wa timu wana wajibu mkubwa kwa nafasi yao kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa,
mfano; kuhudumia kambi ya wachezaji.
Inapofika
muda wa uwanjani, makocha pekee na wachezaji ndio wenye wajibu wa kulipa
fadhili za viongozi wao na mashabiki waliopo nyuma yao.
Kutokana
na ubora wa Yanga katika kikosi chao, mashabiki wake waliamini Mgambo lazima
wale kipigo kikali jijini Tanga.
Ikimbukwe
kabla ya mechi hiyo, Yanga walitoka kushinda mabao 5-0 dhidi ya Tanzania
Prisons.
Kwa
tafsiri hiyo, safu ya ushambuliaji ya Yanga ilionekana kuwa na uchu mkubwa wa
kufumania nyavu, hivyo watu wengi walitegema kuona karamu nyingine ya mabao
dhidi ya timu ya Mgambo inayoonekana kuwa dhaifu msimu huu.
Juma Kaseja yupo kambini pamoja na mlinda mlango Deo Munish "Dida" aliyekua majeruhi kwa takribani wiki tatu kufuatia kupata jeraha katika mkono wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Kwa
watu wanaojua mpira, kama hawakuthubutu kusema Yanga wana asilimia zote
kushinda mechi ile, bali waliwapa asilimia nyingi ya kupata matokeo mazuri zaidi
ya Mgambo.
Kuipa
timu asilimia kubwa ya ushindi kwasababu ya ubora wa kikosi, ni suala la
kawaida sana hata huko duniani.
Ndio
maana Manchester United walitaniwa kuwa wanaenda kupambana na Bayern Munich
yenye kazi nyepesi ya kuvuna ushindi.
Wengine
walisema ni vita ya Daudi na Goliathi, lakini wakasahau kuwa mpira wa miguu una
matokeo ya aina yake.
Man
United walikuwa na haki ya kupata matokeo yale, hata kama Bayern ni bora zaidi
yao kwa sasa.
Haimaanishi
timu fulani kuwa na kikosi dhaifu, basi haina haki ya kushinda. Soka la
uwanjani linahitaji mipango. Ukipata nafasi tumia.
Mgambo
JKT walikuwa na haki ya kushinda licha ya kucheza pungufu kwa dakika 60 baada
ya mchezaji wao Mohamed Hussein Neto
kuoneshwa kadi nyekundu.
Walionekana
kukomaa zaidi na kuwa na mipango mizuri na ndio maana waliweza kuwafunga Yanga.
Kinachoonekana
kwa baadhi ya mashabiki wa Yanga ni kuamini timu yao ina haki ya kushinda
katika kila mechi kwasababu ya ubora wa
kikosi chao.
Lakini
mpira huwa hauendi hivyo, kufungwa kupo hata kama una ubora mkubwa.
Mara
ngapi timu ndogo zinapata matokeo mbele ya timu kubwa?. Mpira huwa hauna fomula
ya kushinda mechi zote.
Kipigo
cha Mgambo kimezidi kuibua mengi. Mojawapo ni tuhuma za baadhi ya wachezaji
kula rushwa kupoteza mchezo.
Si
rahisi kubaini kama kweli wanaotuhumiwa walikuwa rushwa, kwasabau jambo hili hufanyika kwa siri na
ushahidi unahitajika unapolisema.
Kuna
wakati Azam fc walijiingiza mkenge wa kuwatuhumu kula rushwa Erasto Nyoni, Said Morad na Aggrey Morris na kusababisha
timu kufungwa.
Watu
wa mpira wanakumbuka kesi hii ilifikishwa
mpaka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), lakini baadaye
ushahidi ulikosekana na kuwaachia huru.
Azam
fc walijikuta wakipoteza muda mwingi na kuigharimu timu bila sababu yoyote ya
msingi.
Kelvin Yondani hakuungana na wenzake kambini baada ya kuomba kupumzika na kutatua matatizo yake ya kifamilia, Benchi la Ufundi walimpa ruhusa hiyo kwa kuzingatia mchezaji mwenyewe asingeweza kutumika kwa mchezo wa jumapili dhidi ya JKT Ruvu kufuatia kuwa na kadi tatu za njano, ataungana na wenzake mara baada ya tu ya mchezo huo.
Kuwatuhumu
wachezaji kula rushwa imekuwa tamaduni ya Simba na Yanga, lakini msimu huu
viongozi wa Yanga wameonekana kuwa makini na kukanusha kila inapotokea taarifa
kama hizi.
Wengine
wamekuwa wakiandika na kusema mitaani kuwa baadhi wa wachezaji wa Yanga ambao
ni Athumani Idd `Chuji` , Kelvin Yondani na Juma Kaseja wamesimamishwa
kwasababu ya tuhuma za kuhujumu timu kwenye mechi dhidi ya Mgambo.
Duru
za habari kutoka Yanga zimesema kuwa uongozi wa klabu hiyo unasikitishwa na
taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya Habari tangu siku ya jumatano
kwamba wachezaji Kaseja, Yondani, na "Chuji" wamefukuzwa kwenye timu
na Emmanuel Okwi ameondoka kurejea kwao nchini Uganda.
Yanga
wamesema taarifa hizi ni uongo mtupu, na zina lengo la kuwagawa wachezaji.
“Hakuna
mchezaji yoyote aliyefukuzwa kwenye timu baada ya kupoteza mchezo dhidi ya
Mgambo Shooting mwishoni mwa wiki, taarifa hizo zinasambazwa kwa Propaganda ili
kuweza kuvunja umoja uliopo ndani ya timu kwa wachezaji na walimu, pia kwa Viongozi na wanachama”. Ilisema
taarifa ya Yanga.
Taarifa
hiyo ilizidi kufafanua kuwa Kelvin Yondani hakuungana na wenzake kambini baada
ya kuomba kupumzika na kutatua matatizo yake ya kifamilia.
Benchi
la Ufundi lilimpa ruhusa hiyo kwa kuzingatia mchezaji mwenyewe asingeweza
kutumika kwa mchezo wa jumapili dhidi ya JKT Ruvu kufuatia kuwa na kadi tatu za
njano, lakini ataungana na wenzake mara baada tu ya mchezo huo.
Pia
Athumani Idd "Chuji", David Luhende pamoja na kiungo Haruna Niyonzima
ni wagonjwa, wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanakua `fiti` na kuungana na
wachezaji wao mara baada ya mchezo wa siku ya jumapili.
Aidha
taarifa hiyo ilisema kuwa Juma Kaseja yupo kambini pamoja na mlinda mlango Deo
Munish "Dida" aliyekua majeruhi kwa takribani wiki tatu kufuatia
kupata jeraha katika mkono wakati timu ikijiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa
Sugar.
Athumani Idd "Chuji", David Luhende pamoja na kiungo Haruna Niyonzima ni wagonjwa, wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanakua fit na kuungana na wachezaji wao mara baada ya mchezo wa siku ya kesho
Pia
Emmauel Okwi yupo jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu kufuatia
kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo mwishoni mwa wiki, awali Okwi
aliiumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje na machela.
Kimsingi
viongozi wa Yanga wanapokanusha taarifa hizi, unaweza kugundua kuwa wanaelewa
kuwa soka huwa lina matokeo kama waliyopata kule Tanga.
Kuwatuhumu
wachezaji kunawafanya wawe na msongo wa mawazo na kubeba mzigo mzito kichwani.
Emmauel Okwi yupo jijini Dar es salaam akiendelea na matibabu kufuatia kutonesha goti katika mchezo dhidi ya Mgambo mwishoni mwa wiki, awali Okwi aliiumia katika mchezo dhidi ya Prisons na kutolewa nje na machela.
Ufanisi
wao unapungua wanapokuwa uwanjani, kwasababu wanacheza kuogopa kukosea.
Kama
ni mshambuliaji anaweza kuogopa kujaribu kupiga mashuti kwa hofu ya kukosa bao
na kutuhumiwa kula rushwa.
Kama
ni mlinda mlango anashindwa kujiamini akiwa langoni, na ikitokea akafungwa bao,
basi anajivuruga zaidi.
Si
wakati muafaka kwa wanayanga kuanza kutuhumiana kwa mambo ya rushwa ikizingatiwa
wana kibarua kizito kuteteta ubingwa wao.
Wanapolumbana
muda huu na kuwasema vibaya wachezaji wao, wanaingiza balaa katika kikosi chao.
Mbele
yao wapo Azam fc waliopo katika hali tulivu zaidi. Kuwang`oa kileleni umakini
mkubwa na jitihada vinahitajika.
Yanga
wakubali matokeo ya uwanjani na wajiandae kufungwa kwani mpira ndivyo ulivyo.
Hawana
haki ya kushinda tu, hata kupoteza pia. Hivyo
lazima wajifunze kuwa watulivu wanapoharibu ili kujipanga kwa mchezo mwingine.
Kutuhumiana
kwa mambo ya rushwa si wakati wake kwasasa.
0 comments:
Post a Comment