Na
Baraka Mpenja , Dar es
salaam
0712461976
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wapo katika msongo
wa mawazo baada ya kuweka rehani ubingwa
wao msimu huu mbele ya wana Lambalamba Azam fc wanaotesa kileleni kwa pointi
53.
Ligi
ikiwa katika hatua za mwisho, Yanga wanaonolewa na kocha mkuu, Mholanzi, Hans
Van Der Pluijm wamebakiza mechi 4 tu ambazo sawa sawa na dakika 360.
Katika
msimamo, Yanga wapo nafasi ya pili baada ya kushuka dimbani mara 22 na
kujisanyia pointi 46, pointi 7 nyuma ya Azam fc.
Dakika
360 zilizosalia kwa Yanga zitawafanya wawe watumwa kwasababu ya kasi ya Azam fc
waliopo kileleni.
Wana
Lambalamba wameshuka dimbani mara 23 na hawajawahi kupoteza mchezo hata wowote.
Kwa
matokeo hayo, Azam fc wanasalia kuwa timu bora zaidi msimu huu kwa maana ya
matokeo ya uwanjani.
Wakati
mwingine, mpira wa miguu una matokeo yasiyotabirika, hasa ushindi unapokuwa
muhimu kwa klabu yoyote ili kuamua hali fulani, mfano kutwaa ubingwa au kukwepa
kushuka daraja.
Kwa
kawaida, timu moja inapotangulia kufunga bao katika mchezo, inamfanya mwenzake
kuwa mtumwa.
Kwa
fomula nyepesi, huwezi kuandika mbili bila moja. Unapofungwa bao 1-0 dakika ya
1, utakuwa mtumwa wa dakika 89 kutafuta njia ya kusawazisha na hatimaye
kuandika bao la pili na la ushindi.
Ukiangalia
msimamo wa ligi kuu mpaka sasa, Yanga wamebaki kuwa watumwa wa uwanjani zaidi
ya klabu yoyote.
Utumwa
wao upo katika mazingira mawili ambayo yanaonekana kufanana, lakini yana
utofauti.
Mosi;
ni watumwa wa kuhitaji kutetea ubingwa wao katika ligi yenye ushindani mkubwa
zaidi.
Ili
kuendeleza heshima yao, wanalazimika kujituma kwa ngvu zote katika michezo
minne iliyosalia, ili kufanikisha malengo yao.
Kupata
ubingwa ni jambo zuri, lakini unapotetea msimu unaofuata, inakuwa nzuri zaidi
na unadhihirisha kuwa hukubahatisha kutwaa taji.
Pili;
Yanga ni watumwa wa kuhitaji kusawazisha pointi 7 walizopo nyuma ya Azam fc ili
kuweza kutetea ubingwa wao.
Wakati wakiwa katika mazingira hayo magumu,
Azam fc nao wanajitahidi kuziba njia za kukamatwa na Yanga.
Njia
inayotumika na Azam fc ni kuhakikisha wanashinda mechi zote tatu zilizosalia.
Tayari
Azam fc wapo mbele dhidi ya Yanga, kwa maana nyingine unaweza kusema Yanga ni
watumwa wa vinara hao wa ligi kuu.
Hawana
namna ya kutetea ubingwa bila kusawazisha pengo la pointi saba na kuwaombea
Azam fc wafanye vibaya.
Kama
Yanga watashinda mechi zote nne zilizosalia, wataweza kufikisha pointi 58,
wakati Azam nao wana uwezo wa kuzifikia na zaidi.
Azam
wamebakiza mechi tatu, kama watashinda zote watafikisha pointi 62. Kwa pointi
hizo, hata Yanga wakishinda michezo yote kwa mabao 100, bado ubingwa utatua
Chamazi.
Kwa
matokeo yanayopatikana mechi hizi za mwisho, huwezi kutegemea Yanga na Azam fc
kushinda mechi zao zilizosalia.
Kumbuka
jumapili Yanga wanakabiliana na JKT Ruvu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Huu
utakuwa mtihani mwingine wa Pluijm kuanza
rasmi utumwa wa kuwafukuzia Azam fc kileleni.
JKT
Ruvu wapo nafasi ya 9 kwa pointi 28. Kiukweli wapo mazingira tata ya kushuka
daraja, kwa maana hiyo wanatakiwa kupambana kwa nguvu zote kupata pointi tatu
mbele ya Yanga .
Kuwafahamu
wapinzani wako kunakufanya uongeze maarifa ya kuwakabili.
Kocha
wa JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro anawafahamu wachezaji wote wa Yanga kwasababu
alikuwa nao mzunguko wa kwanza.
Iliwafundisha
akiwa kocha msaidizi, na kuna wakati aliwafundisha bila uwepo wa kocha mkuu, Ernies
Brandts.
Mchezo
wa jumapili utakuwa mgumu kwa timu zote mbili. Yatahitajika maarifa makubwa kwa
makocha wote wawilli kupata ushindi.
Yanga
wataingia wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 na Mgambo JKT , wakati JKT
Ruvu walishinda mechi yao ya mwisho dhidi ya Rhino Rangers kwa mabao 3-1.
Utumwa
wa pili wa Pluijm utakuwa aprili 9 mwaka
huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Kagera Sugar.
Wakata
miwa hawa wa Kaitaba, hawahitaji ubingwa wala nafasi ya pili. Malengo yao ni
nafasi ya tatu na nne.
Kama
wana malengo hayo, basi wamejipanga na wanaendelea kujipanga ili kufanya vizuri
katika michezo yao minne iliyosalia kuanzia wa leo dhidi ya Simba sc.
Bila
shaka mechi hii ya Yanga na Kagera itakuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote.
Haitakuwa
rahisi kwa Pluijm kuchomoka katika mechi hii, lakini akiwa na mipango safi
ataweza kuvuna pointi tatu muhimu.
Baada
ya mechi hiyo, Yanga sc watasafiri kwenda mkoani Arusha kuwakabili JKT Oljoro
aprili 13 mwaka huu kwenye uwanja wa Shk. Amri Kaluta Abeid.
Endapo
kwa wakati huo JKT Oljoro watakuwa kwenye nafasi nzuri ya kubakia ligi kuu, basi itakuwa mechi ngumu kwa Yanga.
Kwakuwa
Oljoro mpaka sasa wapo nafasi ya 13 kwa kushuka dimbani mara 23 na kujikusanyia
pointi 15 pekee, wanahitaji kujidhatiti kushinda mechi zote tatu walizosalia
nazo, japokuwa inaonekana haitawasaidia kubakia.
Oljoro
wapo katika hatari zaidi ya kushuka daraja, lakini haimaanisha Yanga watakuwa
na kazi rahisi kuibuka na ushindi. Mipango mzuri ya uwanjani itahitajika.
Mechi
ya mwisho ya Yanga itakuwa aprili 19 dhidi ya mahasimu wao wakubwa, Simba Sc.
Mechi
ya watani haitabiriki kirahisi, bali matokeo yanaamriwa ndani ya dakika 90.
Mechi
hizi nne zilizosalia, zimewaweka Yanga katika mazingira ya utumwa zaidi ili
kutetea ubingwa wao.
Azam
fc wao wamebakiza mechi dhidi ya Ruvu shooting, Mbeya City na JKT Ruvu.
Ruvu
Shooting hawapo nafasi ya hatari katika msimamo, lakini wataingia kwa lengo la
kulinda heshima na pengine kuhitaji kuwa timu pekee kuanza kuvuruga rekodi ya
Azam ya kutofungwa msimu huu.
Timu
ya kuharibu rekodi ya Azam fc haijapatikana, na kinachosubiriwa ni klabu hizi
tatu zilizobakiza mechi nao.
Kocha
wa Azam fc, Joseph Marius Omog anahitaji kujiandaa vyema kwenda kuvuna pointi tatu kwa Ruvu Shooting
kule Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Atahitaji
kuwa na tahadhari kubwa kama kweli anataka kutwaa ubingwa.
Pia
mechi ya Azam fc na Mbeya City itakuwa
na kimuhemuhe zaidi kwasababu City nao wanauwinda ubingwa msimu huu.
Mpaka
sasa City wameshashuka dimbani mara 23 na kujikusanyia pointi 45 pointi moja
nyuma ya Yanga.
Katika
uwanja wa sokoine, Wagonga nyundo hawa wa Mbeya, hawajawahi kufungwa, hivyo
Azam fc watahitaji kujipanga kuvunja rekodi yao.
Mechi
ya mwisho kwa Azam fc itakuwa dhidi ya JKT Ruvu ,na uzito wa mechi hiyo utategemeana na matokeo
ya timu zote katika michezo miwili ijayo.
Kama
JKT Ruvu watakuwa wamefikia hatua nzuri kabla ya mechi ya mwisho, basi inaweza
kuwa msaada kwa Azam fc.
Lakini kama bado watakuwa kwenye mstari
mwekundu wa kushuka daraja, basi itakuwa kibarua kizito zaidi.
Hakika
utumwa wa Yanga katika dakika 360 za michezo minne iliyosalia ni mkubwa sana na
wanahitaji kufuta pengo la pointi 7 dhidi ya Azam fc.
Hakuna
jinsi, Yanga lazima washinde mechi zote zilizosalia, huku wakiomba dua mbaya
kwa Azam fc wapoteze angalau michezo
miwili.
Azam
fc wametangulia mbele kwa pointi, Yanga ni watumwa wa kusawazisha hali hiyo,
hivyo wanatakiwa kuwa na mipango mizito zaidi.
0 comments:
Post a Comment