Kocha wa Young Africans akiongea
na waandishi wa habari jijini Cairo
......................................................
Young Africans kesho itashuka dimba la Uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro majira ya saa 10 jioni kupambana na timu ya wakata Miwa
timu ya Mtibwa Sugar ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom msimu wa 2013/2014.
Mchezo wa kesho utakua
ni mechi ya kwanza ya Ligu Kuu kwa Young Africans kwa takribani wiki mbili
kufuatua kuwa katika mashindano ya kimataifa , mechi inatarajiwa kuwa na
upinzani mkali kufuatia Young Africans kusaka pointi 3 muhimu ili kuweza
kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea Ubingwa wake kwa mara ya pili
mfululizo.
Kocha mkuu wa Young
Africans Hans Van der Pluijm amesema vijana wake wapo fit kuelekea mchezo huo
jana na leo wamefanya mazoezi katika uwanja wa jamhuri na morali ni
hali ya juu kuelekea kwa mchezo huo.
Nimewaandaa vijana
wangu kuhakikisha wanafanya vizuri na kupata ushindi, natambua Mtibwa Sugar
watakua wamejiandaa vizuri pia ila mwisho wa siku timu iliyojiandaa vizuri ndio
itakayoibuka na ushindi.
Mtibwa Sugar ambayo
ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya JKT Ruvu itahitaji kucheza kufa na
kupona ili kuweza kupata pointi 3 muhimu ili iweze kujiweka kwenye
mazingira mazuri ya kuingia kwenye top 4.
Katika mchezo wa kesho
Young Africans itakosa huduma ya kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye ni
majeruhi kufuatia kupata maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa Klabu Bingwa
Barani Afrika dhidi ya timu ya Al Ahly ya Misri.
0 comments:
Post a Comment