Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
0712461976 au 0764302956
MSHAMBULIAJI hatari wa Manchester United, Mholanzi, Robin van Persie amekanusha uvumi ulioenea kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo majira ya kiangazi mwaka huu kufuatia mwenendo mbovu wa kocha David Moyes na amesisitiza kuwa anapenda kumalizia soka lake Old Trafford.
Van Persie aliwapatia ubingwa wa ligi kuu soka nchini England Manchester United katika msimu wake wa kwanza mwaka jana baada ya kununuliwa kwa dau la paundi milioni 24 kutoka Asernal, lakini ameshindwa kung`ara msimu huu chini ya Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson .
Imekuwa ikipendekezwa kuwa majira ya kiangazi mwaka huu, Moyes amuuze RVP ili kutimiza malengo yake ya kukifumua kikosi kizima, na mchezaji anayemuwania kwa nguvu kuimarisha zaidi safu yake ya ushambuliaji ni Edinson Cavani .

Van Persia mwenye miaka 30 alisema anataka kuona miaka yake miwili iliyosalia katika klabu ya Man United ikimalizika salama na ataweza kufuata nyayo za Wayne Rooney kwa kusaini mkataba mpya kwa mara nyingine.
“Ukweli ni kwamba, nina furaha sana kuwepo katika klabu hii”. Alisema katika mahojiano ya maandalizi ya mechi ya jumapili dhidi ya Liverpool.
“Nilisaini miaka minne na natamani kukaa zaidi ya miaka miwili niliyobakiza kwenye mkataba wangu. Hivi ndivyo ninavyojisikia, japokuwa imekuwa ikizungumza tofauti”. Alisema RVP.
Imekuwa ikidaiwa kuwa Van Persia amekatishwa tamaa na kustaafu kwa kocha Ferguson na hafurahishwi na mbinu za ufundisha za Moyes.


Majadiliano: Van Persie akiwa na kocha wake David Moyes katika uwanja wa mazoezi wa Carrington
0 comments:
Post a Comment