Tuesday, March 18, 2014

Dodoma. Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Beatrice Shelukindo, amependekeza Katiba ijayo itoe haki ya kufanya kazi ili vijana wapate nafasi za kazi.
Mjumbe huyo alisema tabia ya watu kufanya kazi hata wakizidi umri wa miaka 60, inapaswa itamkwe kwenye Katiba kuwa ni kosa kisheria.
Shelukindo alitoa kauli hiyo katika mchango wake kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), iliyofanyika katika Ukumbi wa New Dodoma Hoteli.
Warsha hiyo ililenga kuwapa nafasi wabunge wa Bunge la Katiba kuchambua kwa makini mambo muhimu ambayo yanatakiwa kuingia kwenye Katiba ijayo ambayo yanahusiana na haki za binadamu.
“Bado Tanzania tuna tatizo, tena ni kubwa maana watu wanafanya kazi hadi wanafikisha miaka 60 na zaidi huku wakiendelea kupewa mikataba ya vipindi maalumu. Hili ni kosa kubwa kwenye Katiba lazima tuliangalie,” alisema Shelukindo na kuongeza “Angalieni mfano wa mabalozi wetu, yaani wanakwenda wakiwa wazee kiasi ambacho hata uwezo wa kufikiri unakuwa umepotea wakati vijana wanaendelea kusugua soli mitaani pamoja na elimu zao kuwa nzuri,”.
Mbunge huyo alipendekeza Katiba ijayo ipige marufu mtu aliyefikia umri wa miaka 60 kuendelea na kazi na badala yake kustaafu. Iwe ni jambo la lazima ili akafanye kazi binafsi.
Alisema mpango huo ukikubaliwa, unaweza kuwa mkombozi kwa vijana kwani nao watapata kuingia katika ajira na kufanya kazi kuliko kusubiri bila matumaini yoyote.
CHANZO: MWANANCHI

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video