Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
Tel: 0712461976 au 0764302956
MTU aliyesahaulika, Emmanuel Adebayor amepiga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Southampton na kuongeza matumaini ya kocha wa muda wa Tottenham Hospurs Tim Sherwood kupata kazi ya kudumu.
Southampton wakiwa nyumbani walikuwa wa kwanza kutikisha nyavu za Spurs katika dakika ya 13 kupitia kwa Adam Lallana, lakini dakika ya 25, mshambuliaji nyota wa Spurs raia wa Togo, Emmanuel Adebayor aliisawazishia timu yake bao hilo.
Mpaka dakika 45 zinamalizika, ubao wa matangazo ulikuwa unasomeka 1-1.
Kipindi cha pili Spurs walikuja juu ya katika dakika ya 54, Jos Hooiveld alifunga bao la pili, lakini halikudumu kwani dakika tano tu baadaye, Rickie Lambert aliisawazisha bao hilo.
Dakika ya 64, Adebayor aliwainua vitini mashabiki wa Spurs baada ya kufunga bao la tatu na la ushindi.
Spurs waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kula kisago cha mabao 5-0 jumapili iliyopita kutoka kwa Liverpool na kusababisha kocha mkuu Andre Villas-Boas kuoneshwa mlango wa kutokea kabla ya saa 24 kutimia tangu ale kipongo hicho.
Sherwood, aliyekuwa Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa klabu ya Tottenham alikabidhiwa majukumu ya kuongoza kikosi hicho. Alifungwa katika kombe la ligi `Capital One` na West Ham katikati ya wiki, na leo hii Adebayor amempa matumaini baada ya kuongoza timu katika ushindi wa 3-2 ugenini dimba la St Mary.




Kikosi cha Southampton: Gazzaniga 6, Chambers 7, Hooiveld 5, Lovren 6, Fox 5 (Gallagher 78 min); Schneiderlin 6, Davis 6 (Ramirez 69, 5), Cork 6 (Ward-Prowse 63, 6); Lallana 8, Lambert 6, Rodriguez 5.
Kikosi cha Spurs: Lloris 6; Walker 7, Dawson 7, Chiriches 6, Rose 6; Lamela 5 (Chadli 60, 7), Eriksen 6, Dembele 5 (Bentaleb 50, 7), Sigurdsson 6; Adebayor 8, Soldado 6 (Defoe 85).


Katika mchezo mwingine, Swansea City wakiwa nyumbani wamefungwa mabao 2-1 dhidi ya Everton.
Everton walikuwa wa kwanza kuliona lango la wenyeji wao katika dakika ya 66 kupitia kwa Seamus Coleman akipokea pasi kutoka kwa James McCarthy.
Bryan Oviedo katika dakika ya 70 aliisawazishia Swansea bao hilo, lakini jahazi lao likazama dakika ya 84′ kupitia kwa Ross Barkley
0 comments:
Post a Comment