Kocha wa Yanga, Ernie Brandts (Kushoto) wakiwa na msaidizi wake, Fredy Ferlix Minziro (Kulia)
Na Braaka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans wamebeza
watani zao wa jadi , Wekundu wa msimbazi Simba Sc kwa mwendo wao wa
kusuasua na kuwatoa katika Kinyang`anyiro cha ubingwa msimu huu.
Kocha
msaidizi wa Yanga, Fredy Ferlix Minziro, Catalaiya Majeshi baba Isaya,
amesema mbio za ubingwa ni baina yao na Azam kwani Simba wameshajitoa
kwani kikosi chao kina matatizo mengi, na kwa upande wa Mbeya City
amesisitiza kuwa hawana uwezo wa kupambana mpaka mwisho, hivyo mzunguko
wa pili watalegeza kamba na kuwa timu ya kawaida sana.
“Ligi
ni ya kawaida sana ingawa kuna ushindani kiasi fulani, msimu uliopita
tulimaliza mzunguko wa kwanza tukiwa na pointi 29 na msimu huu
tutamaliza tukiwa nazo 28. Katika mbio za ubingwa Simba wameshajitoa,
kwahiyo timu zinazowania ni Yanga na Azam, na si timu yoyote”. Alisema
Minziro.
Minziro
alisema mzunguko wa pili Mbeya City watalegea kwani watakutana na
vijana wenzao ambao sasa wataingia uwanjani kwa kushindana nao na
kuondoa mawazo kuwa ni timu ndogo iliyopanda ligi kuu.
“Mbeya
City imepanda daraja juzi juzi tu, kila timu ilipokuwa inakutana nayo
ilikuwa inachukulia kama timu ndogo tofauti na timu za Simba na Yanga,
Mzunguko wa pili watakumbana na changamoto kubwa na lazima wawaache
Yanga na Azam fc katika mbio za ubingwa”. Aliongeza Minziro.
Kocha
huyo na mchezaji wa zamani wa Yanga, aliongeza kuwa timu ndogo
zinapokutana na timu kubwa huwa zinatoa macho yao kwa nguvu zote, lakini
zikikutana zenyewe huwa zinacheza soka la kawaida.
Akizungumzia
mchezo wa kufunga pazia la mzunguko wa kwanza wa ligi kuu bara dhidi ya
JKT Oljoro uwanja wa Taifa Alhamisi (Novemba 7 mwaka huu), Minziro
alisema kikosi kinaendelea vizuri, wachezaji wote wapo katika morali
kubwa na wanajiandaa kuwainua vitini mashabiki wao watakaofurika
dimbani.
“Ninachowaambia
wana Yanga ni kuwa pamoja na kiwasapoti wachezaji wao, kuna wana Yanga
wachache ambao wanafanya mambo ambayo si ya kimpira, mara wanawazomea
wachezaji wao, waache mara moja tabia hii”. Alisema Minziro.
Yanga
kwa sasa wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi zao 25, wakati Mtani wao
Simba yupo nafasi ya nne na pointi 21, na katika nafasi ya kwanza Azam
fc wanabarizi wakiwa na pointi 26 sawa na Mbeya City waliopo nafasi ya
pili lakini wanazidiwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
0 comments:
Post a Comment