Na Mwandishi Wetu
MSANII
Upendo Nkone amekuwa wa kwanza kuthibitisha kushiriki Tamasha la
Krismas litakalofanyika Desemba 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema jana kuwa
tayari wamefikia makubaliano na msanii huyo na kwamba bado wanaendelea
na mazungumzo na wasanii wengine wa nje na ndani kuhakikisha tamasha
hilo la nyimbo za kumsifu mungu linakuwa zuri.
“Nafurahi
kuwajulisha wapenzi wa muziki wa kiroho kuwa kamati yangu tayari
imefikia makubaliano na Nkone, hivyo mambo yatakuwa mazuri kadri siku
zinavyokaribia,” alisema Msama.
Baadhi
ya nyimbo za msanii huyo ni Upendo wa Yesu, Hapa Nilipo, Mungu Baba,
Yesu Aliniita, Sikiliza Nikuambie, Usiogope, Ijaposema, Uumbaji, Yesu
Nakupenda, Kanisa na Habari Njema.
Nyimbo nyingine ni Niacheni Niimbe, Nimebaki na Yesu, Uniongoze Yesu, Nakuhitaji, Acha Uovu, Yesu Atakutunza na Moyo Wangu.
Tamasha
la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es
Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.
Kwa
mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la
Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania na
kwamba litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu.
0 comments:
Post a Comment