Meneja
Uhusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele
akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maazimo
yaliyofikiwa kwenye mkutano wa 23 wa wanachama na wadau wa mfuko huo
uliofanyika Arusha October mwaka huu ambapo moja ya maazimio ni waajiri
kuwapa fursa wafanyakazi wao kujiunga na mifuko ya hifadhi ya
jamii.katikati ni Meneja Uwekezaji wa mfuko huo Bw. Selestine Some na
Mwishoni ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi. Fatma Salum.

Meneja
Huduma kwa Wateja na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bw. Godfrey
Mollel akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mpango wa mfuko
huo kufikisha wanachama 400,000 ifikapo mwaka 2015, kwa sasa mfuko huo
una wanachama takribani 300,000,kushoto ni Meneja Uhusiano na Masoko wa
Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.

Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano na Mfuko wa Pensheni wa
PPF katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Hassan Silayo- MAELEZO
Na Hassan Silayo-Maelezo
Waajiri nchini wametakiwa kuwa utaratibu
wa kutoa mafunzo elekezi kwa waajiriwa kuhusu namna ya kujiandaa na
maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi anapoingia katika ajira.
Wito huo umetolewa na meneja uhusiano na masoko wa mfuko wa pensheni wa PPF Lulu mengele wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini dar es salaam.
Megele alisema kuwa kumekuwa na tabia ya waajiriwa kusahau kujiwekea akiba na hivyo kusababisha matatizo wakati wa kustaafu.
”napenda
kuwaasa waajiri waanzishe utaratibu wa kutoa mafunzo elekezi kuhusu
namna ya kujiandaa na maisha ya kustaafu tangu siku mfanyakazi
anapoingia katika ajira hii itamsaidia mfanyakazi kuwa na mipango ya
maandalizi kabla ya kustaafu na sio kusubiri mtu astaafu ndio aanze
kuweka mipango ya maisha yake”. Alisema Mengele.
Pia
Menegele aliongeza kuwa kuna haja ya waajiri nchini kuwapa fursa
Wafanyakazi wapya kujiunga na Mifuko mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii.
“napenda
kuwaasa waajiri wote nchini kuwapa fursa wafanayakazi wapya kujiunga na
mifuko ya hifadhi ya jamii kwani kwa kufanya hivi kutaweza kuwasaidia
wafanyakazi kuwa na uwezo wa kujikimu na kukabiliana na changamoto za
maisha katika siku za baadae” alisema Mengele.
Akieleza
mipango ya kuongeza wanachama meneja wa huduma kwa wateja na wanachana
Godfrey Mollel alisema wanamipango ya kuongeza wanachama hadi kufikia
400,000 ifikapo mwaka 2015.
“kwasasa
tuna wanachama 300,000 lakini kutokana na ubora wa huduma za PPF
tunategemea kuongeza idadi ya wanachama hadi kufikia 400,000 ifikapo
mwaka 2015.
Mfuko
wa pensheni wa PPF unajivunia kutekeleza majukumu yake kwa asilimia 80
kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mwasiliano(TEHAMA).
0 comments:
Post a Comment