Katibu
Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome
akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa hafla ya utambulisho
wa Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda Shuleni leo
jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Mradi wa Kupeleka Bustani za
Mbogamboga na Matunda Shuleni Dkt. Usha R. Palaniswamy.
Meneja
Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda Shuleni Dkt. Usha R.
Palaniswamy akifafanua jambo wakati wa utambulisho wa Mradi huo, hafla
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa Elimu ya
Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi. Paulina Mkonongo
na Mratibu wa Mradi Tanzania Bi. Joyce Sekimanga.
Mkurugenzi
wa Elimu ya Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi.
Paulina Mkonongo akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi(hawapo pichani) wakati wa hafla ya utambulisho wa
Mradi wa kupeleka Bustani ya Mbogamboga na Matunda shuleni leo jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Mratibu wa mradi huo Bi. Bi Joyce Sekimanga
Mkurugenzi
wa Elimu ya Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bi.
Paulina Mkonongo akisisitiza jambo kwa watumishi wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi(hawapo pichani) wakati wa hafla ya utambulisho wa
Mradi wa kupeleka Bustani ya Mbogamboga na Matunda shuleni leo jijini
Dar es Salaam.Kushoto ni Mratibu wa mradi huo Bi. Bi Joyce Sekimanga
Mmoja
wa watumishi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo akichangia mada baada ya
kutambulishwa Mradi wa kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda leo
jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija – Maelezo
Na Frank Shija
Tanzania
kuwa miongoni mwa nchi chache Barani Afrika zitakazo nufaika na mradi
wa kupeleka bustani za mbogamboga na matunda shule.
Hayo
yamebainika wakati wa hafla ya utambulisho wa mradi huu ilyofanyika leo
jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome
Akizungumza
katika hafla hiyo Katibu Mkuu huyo amesema kuwa ni fursa nzuri kwa
Tanzania kufikiwa na mradi huu kwa kuwa utasaidi kuongeza hamasa ya
kutumia mboga za majani na matunda miongoni mwa jamii.
Aidha
Prof. Mchome ameongeza kuwa ni Serikali imepoke mradi huu na kuhadi
kushirikiana na wadau wengi katika kuhakikisha mradi huu unaendelea.
”
Tumepokea kwa faraja kubwa mradi wa kupeleka bustani za mbogamboga
mashule, nami naamini kuwa wanafunzi wetu watafurahi sana kwani
utawaongezea maarifa lakini pia ziada inaweza kuuzwa na kutatua matatizo
yao” Alisema Prof. Mchome.
Prof.
Mchome aliongeza kuw utekelezaji wa mradi huu utashirikisha Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kwa
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa Kupeleka Bustani za Mbogamboga Shuleni Dkt.
Usha R. Palaniswamy amesema kuwa kutokana na umuhi wa virutubisho
vilivyopokatika mbog za majani na matunda taasisi yake iliamua kusaidi
kuhamasisha matumizi yake kadri iwezekanavyo.
Dkt.
Usha aliongeza kuwa kwa kupeleka mradi huu katika ngazi ya shule za
Sekondary kutaleta hamasa kubwa kwa jamii kwa kuwa vijana wengi wa
Sekondary ndiyo hao hao wanategemewa na familia zao.
Aliongeza
kuwa nifaraja kwake kuona Tanzania inakuwa nchi ya pili katika
utekelezaji mradi huu bara Afrika, kwani richa ya Tanzania pia
unatekelezwa Burkinafaso kwa sasa na umefanikiwa sana.
Wakati
huo huo Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari Bi. Paulina Mkonongo , amesema
kuwa anaishukuru taasisi ya AVRDC ambao ndio walioleta mradi huu hapa
nchi kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na Serikali kwa kutekeleza baadhi
ya program ambazo zilikuwa zimeanza muda murefu.
Bi.
Mkonongo amesema kuwa mradi huu utaongeza kasi na kuleta hamasa kwa
wanafunzi na wazazi kujijengea utamaduni wa kulima bustani itakayo wapa
faida mara mbili kwa kuwa watapata mboga na matunda wakati huohuo
kujipatia kipato kama ziada.
Mradi
wa kupeleka Bustani za Mbogamboga na Matunda unatarajiwa kuanza mapema
mwezi wa kwanza 2014,utatekelezwa katika jumla ya shule za Sekondari 30
mkoani Morogoro,na baadae utasamba nchi nzima baada ya kuonyesha
mafanikio katika awamu hii ambayo itakamilika mwishoni mwa mwaka 2015.



0 comments:
Post a Comment