Kiongozi
Mkuu wa Kanisa la Christ Embassy Mchungaji Ken Igini akisisitiza jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, juu
ya huduma ya afya itakayotolewa na kanisa hiloKesho katika viwanja vya
Biafra, kulia ni Mchungaji Fredy Rwegasira.
Mchungaji
Abrahim Kiyinga toka Kanisa la Christ Embassy (kushoto) akisistiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,
juu ya huduma za afya zitakazotolewa na kanisa hilo siku kesho katika
viwanja vya Biafra, katikati ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Christ
Embassy Mchungaji Ken Igini na mwisho ni Mchungaji Fredy Rwegasira.
Mchungaji
Abrahim Kiyinga toka Kanisa la Christ Embassy (kushoto) akisistiza
jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,
juu ya huduma za afya zitakazotolewa na kanisa hilo siku kesho katika
viwanja vya Biafra, katikati ni Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Christ
Embassy Mchungaji Ken Igini na mwisho ni Mchungaji Fredy Rwegasira.
Baaadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Kiongozi Mkuu wa Kanisa
la Christ Embassy Mchungaji Ken Igini (hayupo pichani) wakati akielezea
juu ya huduma ya afya itakayotolewa na kanisa hiloKesho katika viwanja
vya Biafra.
Picha zote na Eliphace Marwa – MAELEZO
Na Eliphace Marwa – Maelezo
Kanisa
la Christ Embassy linatarajia kuendesha zoezi la kutoa huduma za afya
kwa wakazi wa Dar es Salaam siku ya kesho katika viwanja vya Biafra,
kinondoni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa
Kanisa hilo Tanzania Mchungaji Ken Igini amesema kuwa lengo la kutoa
huduma hiyo ya afya kwa wakazi wa Dar es Salaam ni sehemu ya
kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi mkuu wa kanisa hilo duniani
Mchungaji Chriss Oyakhilome.
“Kanisa
la Christ Embassy limeamua kutoa huduma ya afya kwa wananchi ikiwa ni
sehemu ya kusherehekea kuzaliwa kwa kiongozi wetu mkuu Mchungaji Chriss
Oyakhilome”, alisema Mchungaji Ken Igini.
Aidha
Mchungaji Ken aliongeza kuwa ni imani yao kuwa watu watajitokeza kwa
wingi kwani matarajio yao ni kuhudumia zaidi ya watu elfu moja kwani
kutakuwa na madaktari wa kutosha kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
“Tunatarajia
kupata wataalam kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo wizara ya afya na
taasisi zingine ambazo zimeonesha nia ya kushirikiana na kanisa la
Christ Embassy katika kutoa huduma hii kwa watanzania wenye mahitaji”,
alisema Mchungaji Ken Igini.
Naye
Mchungaji Abrahim Kiyinga alisema kuwa endapo watu watajitokeza kwa
wingi wataongeza siku ya kutoa huduma ya afya kwa watu wenye shida ya
kupata huduma hiyo.
“Ni
matarajio yetu kuwa watu watakuja kupima kwa wingi sana kwani huduma
hizi ni bure kabisa na tutaanza kutoa huduma za vipimo vya magonjwa
mbalimbali kuanzia saa tatu asubuhi”, alisema Mchungaji Abrahim Kiyinga.
Sherehe
hii ya kuazaliwa kwa Kiongozi mkuu wa kanisa la Christ Embassy
zinasherehekewa na makanisa yote ya Christ Embassy Dunianiani kwa
kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku hiyo.


0 comments:
Post a Comment