Mrembo
wa Taifa Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa yuko Kampala
Uganda kwa mwaliko rasmi kutoka kampuni ya Arapapa Fashion House &
Design ya nchini Uganda.
Redds
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa atakuwepo nchini Uganda kwa
muda wa siku 5 hadi tarehe 9 Novemba 2013 anatarajiwa kurejea nchini.
Akiwa
nchini Uganda ataungana na warembo wengine kutoka nchi za Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, Kenya, Rwanda, Burundi na wenyeji Uganda.
Pamoja
na mambo mengine warembo hao watahusika pia katika kazi za jamii na
baadaye kupanda jukwaani pamoja katika onyesho la mavazi lililoandaliwa
na Kampuni hiyo.
Kampuni ya Arapapa imekuwa ikifuatilia kwa karibu mashindano ya urembo ya Miss Tanzania tangu mrembo Happiness anyakue taji na waliazimia kumualika mrembo huyo kutembelea Uganda, jambo ambalo wamelitimiza.
Redds Miss Tanzania 2013 ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Juu katika Chuo cha Strathclyde nchini Scotland, ameamua kuahirisha masomo yake kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi hapo atakapovua taji mwishoni mwa mwaka 2014.
Mrembo Happiness Watimanywa atawakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia hapo mwakani.
0 comments:
Post a Comment