Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid
………………………………………………………………………………………
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imeitaka Serikali kupitia
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwasilisha haraka muswada wa Sheria
ya Bima ya Afya kwa watanzania wote ikijumuisha makundi maalumu ya
wazee, watu maskini na walemavu wasio na uwezo ili wanufaike na huduma
zinazotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Agizo
hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bi.
Jenista Mhagama wakati akifungua semina ya Bima ya Afya kwa wajumbe wa
kamati hiyo mjini Dodoma.
“Sisi
kama Kamati tumedhamiria kwamba Watanzania wote wapate huduma za
matibabu kupitia utaratibu huu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani
ndio wenye manufaa makubwa kwa wanajamii,” alisema.
Akitoa
maelezo ya utangulizi katika Semina hiyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa
Jamii, Dk. Hussein Mwinyi alisema kuwa tayari ameiagiza Bodi na
Menejimenti ya Mfuko kuandaa mapendekezo hayo ili kuhakikisha muswada wa
Sheria ya Bima ya Afya unaandaliwa haraka na kuwasilishwa kwa Serikali
haraka iwezekanavyo.
Naye
Mbunge wa Viti maalumu Bi. Hokololo ameipongeza Bodi na Menejimenti ya
Mfuko kwa hatua na kazi nzuri inayofanya katika kutekeleza majukumu
yake. Alisema
sasa ni muda muafaka kwa menejimenti ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
kuangalia upya suala la uhaba wa dawa kwa kushirikiana na Bohari Kuu ya
Dawa.
Akichangia
mada, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameupongeza Mfuko huo kwa
kazi nzuri lakini ametoa angalizo kwamba juhudi zinazofanywa na Mfuko
huo hazitakuwa na maana kama Watumishi wa Sekta ya Afya hawatakuwa na
utu kwa wagongwa wakati wa kutoa huduma.
Aidha ameishauri serikali kuangalia upya namna ya kuboresha motisha kwa watumishi katika sekta ya afya.
Naibu
Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid kitoa ufafanuzi wa
hoja za ujumla za kisera na hasa kuhusu changamoto ya uhaba wa dawa na
utendaji wa Bohari Kuu ya Serikali Dawa (MSD) imeiambia Kamati hiyo
kwamba kuanzia sasa Dawa zote zitawekwa alama maalumu ya Serikali ili
kuwabaini wale wote wanaohujumu juhudi za Serikali na kwa sasa Serikali
imekwisha kamilisha mchakato wa kuimarisha Mfumo mzima wa utendaji wa
MSD kupitia kwa mkandarasi mshauri aliyepewa kazi hiyo.
Akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya hoja za wabunge, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
huo Bw. Hamisi Mdee amesema tatizo kubwa lililopo katika ufanisi wa
utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii katika Halmashauri ni kutegemea
uongozi wa Mkoa, Halmshauri na Watendaji.
“
Ukiona Mfuko wa Afya ya Jamii unafanya vizuri basi ujue hizo ni juhudi
binafsi za viongozi wa ngazi ya Mkoa na Wilaya kama Mkuu wa Wilaya,
Mkuu wa Mkoa au Wakurugenzi wa Halmashauri na wanapohamishwa tu maeneo
hayo kila kitu hurudi nyuma,” alisema.
Aidha
Kaimu Mkurugenzi huyo, amesema Mfuko wa Bima ya Afya ambao kwa sasa
unasimamia Mfuko wa Afya ya Jamii kwa kutoa ushauri wa Kitaalam
unamkakati wa kuongeza wigo wa huduma za CHF ili zipatikane hadi katika
ngazi ya hospitali za rufaa ngazi ya Mkoa.
“ Hii
itawavutia wanajamii walio wengi kujiunga na taratibu hizi za bima
maana atakuwa na uhakika wa kupata huduma hadi ngazi ya juu badala ya
utaratibu ulivyo sasa’’ amesema bwana Mdee
0 comments:
Post a Comment