Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
KIUNGO
mahiri, mtaalamu wa kupiga pasi na kumiliki gozi akiwa dimbani wa
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara na kikosi cha timu ya
Taifa, `Taifa Stars`, Frank Domayo amewataka vijana wenzake wanaopewa
nafasi na makocha wao kucheza mechi mbalimbali kuonesha juhudi kubwa na
kuzitendea haki nafasi hizo.
Domayo ameuambia mtandao wa MATUKIO DUNIANI
kuwa ligi imekuwa tamu sana kutokana na timu nyingi kuwapa nafasi
vijana ambao wana malengo ya kutafuta maisha na ndio maana wakiingia
uwanjani wanataka kuonekana zaidi , hivyo kupelekea mechi kuwa ngumu.
“Mimi
nafurahi sana kuona vijana wanapewa nafasi, kiukweli wana viwango vya
hali ya juu. Tumemaliza mzunguko wa kwanza tukiwa nafasi ya kwanza,
lakini ligi ni ngumu sana, vijana wana kasi kubwa na wanapamabana sana”.
Alisema Domayo.
Domayo
alisema soka la sasa linahitaji kujituma zaidi kwani ni ajira, hivyo
vijana lazima wajue kuwa mpira wa miguu hauna uchawi, bali ni mazoezi na
kujituma.
“Tusilewe
sifa, tuzingatie programu za mazoezi za makocha wetu, tujitume na kuwa
na utamaduni wa mazoezi binafsi, Kocha mzuri huwa anamtazama mchezaji
mazoezini, hivyo vijana wakipewa nafasi ya kuonesha vipaji vyao
wahakikishe hawafanyi makosa”. Alishauri Domayo.
Kiungo
huyo tegemeo wa Yanga alisema kwasasa wapo mapumzikoni, lakini yeye ana
mikakati yake ya kujiweka sawa kwa ajili ya mzunguko wa pili na
michuano ya kimataifa mwakani.
“Tuna
kazi ngumu ya kutetea ubingwa wetu, pia tunakabiliwa na michuanoi ya
Afrika, lazima nijiweke fiti kwa wakati wote kabla ya kuanza mazoezi ya
pamoja”. Alisema Domayo.
Kinda
huyo amekuwa chaguo la kwanza kwa kocha mkuu wa timu ya Yanga, Ernie
Brandts na amekuwa akicheza mechi nyingi sana kutokana na uwezo wake,
lakini pia ni kivutio kikubwa kwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.


0 comments:
Post a Comment