Kikosi cha timu ya Yanga
Mashabiki
wa timu ya simba yanga wakicheza mchezo wa kuvuta kamba katika kampeni
ya nani mtani jembe na simba kuibuka mshindi wa mchezo huo kwa upande wa
wanaume.
Mashabiki wa simba wakishangilia baada ya kuwashinda yanga mchezo wa kuvuta kamba kupitia bonanza la nani mtani jembe .
Mashabiki
wanawakewa Yanga na Simba wakishindana mchezo wa kuvuta kamba katika
bonanza la nani Mtani jembe lililo fanyika katika uwanja wa majimaji.




Msanii wa kucheza na nyoka akicheza na nyoka katika uwanja wa majimaji kupitia bonanza la nani mtani jembe.
Wasanii wa kikundi cha umoja star maarufu manyoka kikitumbuiza katika Bonanza la nani mtani jembe.

….Bonanza la Mtani Jembe Songea lafunika
….Wananchi wafurika Uwanja wa Majimaji
….Shughuli za Kijamii zasimama kwa muda
…..Yanga yashinda shindano kukimbiza kuku
Na Mwandishi Wetu, Songea
BONANZA
kubwa la NANI MTANI JEMBE ambalo huenda jamii ya Mkoani Ruvuma inaweza
kuliita la kihistoria, limefanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini
Songea limefanyika jana, ambapo mamia ya wananchi walifurika kwa wingi
uwanjani hapo huku mashabiki wa Yanga wakishinda pambano la soka kwa
mabao mawili na shindano la kumsaka na kumkimbiza kuku wa kienyeji huku
Simba wakiibuka kidedea kwenye mchezo wa kuvuta kamba.
Hali
katika uwanja wa Majimaji, maarufu kama wanalizombe ulianza kufurika
majira ya saa nne asubuhi, baada ya wananchi hao wengi wakiwa vijana
kumaliza shughuli za ibada kutoka makanisani.
Mratibu
wa tamasha hilo kwa niaba ya Kilimanjaro Premium Lager, Amedeo Thadeo,
alisema kwamba wameamua kufanya bonanza hilo katika mji wa Songea baada
ya kubaini kuwa mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa yenye mashabiki
wengi wa vilabu vya Simba na Yanga.
Hata
hivyo, michezo kadhaa iliyoanza kufurahisha wananchi waliofurika katika
uwanja huo ulikuwa wa kufukuza kuku tena Jogoo, ambapo washiriki wawili
wapenzi wa klabu za Simba na Yanga walishirikishwa baada ya kuvalishwa
jezi za vilabu hivyo.
Lakini
kwa bahati mbaya, wapenzi wa Simba, walishindwa kuongeza furaha yao
katika uwanja huo, baada ya mshiriki wao kushindwa kumaliza mbio hizo
kwa mafanikio, huku yule wa Yanga Deogras Mwanji, akiibuka kidedea baada
ya kufanikiwa kumkamata jogoo huyo baada ya dakika mbili na sekunde 25.
Hata
hivyo, Mwakilishi wa Mauzo TBL mkoani Ruvuma Masoud Mrisho, aliliambia
gazeti hili kwamba mwamko ulikuwa mkubwa uwanjani hapo, baada ya vijana
walikuja kutoka Dar es Salaam kufanya maonyesho ya promosheni kadhaa
kwenye baa kadhaa mjini Songea.
“Walipokuja
hapa Songea wasanii waliosimamia bonanza hili walianza na kuendesha
promosheni katika baa ya Serengeti, Yapenda Mtini, Delux II, Mamboleo na
kumalizia katika baa ya VALONGO VANGU, mjini Songea na kupata uungwaji
mkono mkubwa kutoka kwa jamii,” alisema Masoud.
Masoud
alisema wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa la bonanza, hivyo kila
kona alikopita yeye na wenzake, walitakiwa kuwahakikishia kwamba bonanza
hilo litafanyika bila kukosa, huku wanenguaji kutoka Bendi za Akudo
Impact Chicharito, na Afande aka Mjeda na Queen Lucy aka Mama Mdogo
wakilipamba jukwaa na kuwaburudisha ipasavyo wananchi waliofurika
uwanjani hapo.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili, umebaini kwamba shughuliza kijamii katika
mji wa songea zilisimama kwa muda kutokana na bonanza hilo, hali ambayo
ilionyesha kuwa wananchi wengi walikuwa na shauku kubwa na bonanza hilo,
japo kuwa wasanii wenyeji wa mji wa Songea walishindwa kuonyesha
umakini wao baada ya kupatiwa nafasi ya kusherehesha jukwaa.
Waliozungumza
na gazeti hili waliipongeza Kilimanjaro Premium Lager kwa bonanza hilo
na kusema limeamsha hamasa ya kimichezo mkoani humo, ambayo imepotea
baada ya timu ya Maji Maji iliyokuwa ikishiriki Ligi Kuu ya Tanzania kwa
miaka kadhaa, lakini ikajikuta ikishushwa daraja baada ya kushindwa
kufanya vizuri.
Bonanza
hilo lililoshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Joseph Mkirikiti,
alionyesha dhahiri ni mshabiki wa Yanga, alipoingia uwanjani
alikabidhiwa jezi ya klabu ya Yanga, na aliamua kusalimia wananchi wote
kwa kluzunguka na kupunga mikono na kuamua kwenda moja kwa moja kukaa
katika jukwaa kuu la uwanja huo, na kuwapongeza wananchi waliojitokeza
katika bonanza hilo akisema amefurahishwa na uratibu wa bia ya
Kilimanjaro Premium Lager kwa shughuli hiyo.
0 comments:
Post a Comment