![]() |
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali , George Masaju |
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
Serikali
imeandaa mafunzo ya majadiliano ya mikataba kwa wataalamu
mbalimbali ili kuwapa mbinu za kuendesha mikataba ya kibiashara
inayohusu rasilimali za nchi kwa manufaa ya Watanzania.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali , George
Masaju wakati wa ufunguzi wa semina ya wiki moja kuhusu majadiliano
ya mikataba inayoendelea kwenye hoteli ya Bahari Beach jijini Dares
Salaam iliyohusisha maaofisa waandamizi wa Serikali kutoka maeneo
tofauti.
“Nchi
yetu hivi sasa iko katika mikakati ya kutumia rasilimali zilizopo kwa
ajili ya maendeleo ya Watanzania kupitia Sheria ya Ubia ya Pamoja
kutoka sekta binafsi(PPP) kwa kuwahusisha wawekezaji wa ndani na nje.
“
Mafunzo haya yawatawasaidia kufanya kazi kwa ufanisi na kuweza
kukabiliana na kampuni kubwa zenye uwezo wa kifedha,katika mikataba
inayohusu madini , mafuta gesi ,nishati, Kilimo kwanza ili kuhakikisha
tunapata faida,” alisema Masaju.
Aliongeza
kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa Dira ya Maendeleo ya Taifa ifikapo
mwaka 2025 Tanzania iwe nchi nyenye kipato cha kati. Hivyo nchi yetu
bado inawahitaji wataalamu kwenye maeneo hayo.
Alisema mafunzo hayo yamehusisha mawakili tisa kutoka katika ofisi hiyo na wengine toka taasisi mbalimbali za umma .
Aliwataka
washiriki wasemina hiyo kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya
kubadilishana mawazo na kupeana uzoefu juu ya suala hilo.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya Uongozi .
0 comments:
Post a Comment