MABINGWA
watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es
salaam wamesema kwa sasa wanaridhishwa na kiwango cha kikosi chao, hivyo
nia yao ni kutetea taji lao msimu huu wenye ushindani mkubwa zaidi.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI,
kocha msaidizi wa klabu hiyo, Fredy Ferlix Minziro amesema kikosi chao
kimeimarika zaidi na wachezaji wote wapo tayari kwa michezo yote ya ligi
kuu.
“Kwa
kawaida tumekuwa tukifanya mabadiliko ya kawaida na ya kimpira kwa
wachezaji wetu, leo utamuona huyo, kesho utamuona mwingine, lakini kuna
watu wanaosema yao kuwa, fulani kaachwa labda alihujumu mchezo wa nyuma,
hapana, ni kawaida kwa makocha kufanya mabadiliko”. Alisema Minziro.
Minziro
alisema mashabiki wengi wa Yanga bado wanasumbuliwa na mzimu wa sare ya
mabao 3-3 dhidi ya Simba, lakini wanatakiwa kujua kuwa ni matokeo ya
kimpira na hakuna wa kulaumiwa zaidi ya kuungana kwa pamoja na safari
yao ya kutetea ubingwa ubingwa wao.
“Ni
kweli kuna makosa ya kimpira yalitokea kwa wachezaji wetu na
kusababisha Simba kusawazisha mabao yote matatu kipindi cha pili, lakini
sisi watu wa mpira huwa tunaamini kuwa makosa siku zote hutoa adhabu na
ndio maana tulipata adhabu ile”. Alisema Minziro.
Minziro
ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga, aliongeza kuwa kwa sasa
wanaendelea na maandalizi ya mchezo wa novemba mosi dhidi ya JKT Ruvu
utakaochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
“Ujue
ligi ya mwaka huu imekuwa na changamoto kubwa, timu zinapambana sana,
kwahiyo na sisi tunajipanga kuhakikisha tunaendeleza wimbi la ushindi na
Mungu atupe uzima zaidi ili kufanikisha malengo yetu”. Alisema Minziro.
Pia
amewasifu wachezaji wao kwa kujituma kwao kwani wametoka nafasi za
nyuma mpaka sasa wapo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu soka
Tanzania bara.
Mechi
iliyopita ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga na Mgambo Shooting
iliyochezwa juzi (Oktoba 29 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
wanajangwani walishinda mabao 3-o na iliingiza sh. Milioni 37,915,000.
0 comments:
Post a Comment