Mashabiki wana mambo: Hawataki kufungwa hata kidogo
Na Baraka Mpenja , Dar es salaam
WEKUNDU
wa Msimbazi Simba SC wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na wana
`Nkulukumbi` Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara
jioni hii uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Simba
ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa nyota wake Amisi
Tambwe, lakini dakika za lala salama, Kagera Sugar walipata penati
iliyofungwa kwa ufundi na mkongwe na beki wa zamani wa Simba, Salum
Kanon.
Hata
hivyo hali ya uwanja iligeuka kuwa shari baada ya mashabiki
wanaodhaniwa kuwa wa Simba kuanza kufanya vurugu na kung`oa viti vya
uwanja wa Taifa hali iliyowalazimu polisi kuwatawanya kwa mabomu ya
machozi.
Hali
hii ilitokea baada ya kusawazishwa kwa bao hilo, kwani inaonekana
mashabiki wa Simba walishajenga imani kuwa wameshinda mchezo huo na
kusahau kuwa soka linahesabika kwa dakika 90.
Shuhuda wa MATUKIO DUNIANI
uwanjani hapo ambaye ni mwandishi wa habari za michezo Mlimani TV na
redio Mlimani ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, Bwana. Fadhili Swala
amesema baada ya kutolewa kwa penati hiyo, mashabiki wa Simba
walionekana kutoridhishwa na kuanza kulaumu.
“Baada
ya Kanon kufunga penati hiyo, mashabiki walionekana kujawa na jaziba na
ndipo walianza kung`oa viti uwanja wa Taifa, lakini kwa sasa hali ni
shwari baada ya polisi kutumia nguvu kuwaamuru kuondoka na kila mtu
amekubali matokeo na kuamua kurejea nyumbani kwake kuendelea na majukumu
mengine. Alisema Swala.
Pia
alisema baada ya kipenga cha mwisho, kocha msaidizi wa Simba Sc,
Jamhuri Kiwhelo `Julio` alionekana kumlaumu mwamuzi wa akiba kuwa
walipunjwa muda.
Swala
aliongeza kuwa mashabiki wengi waliohojiana na mtandao huu pale
uwanjani wameonesha kukerwa na tabia hii ya utovu wa nidhamu kwani mpira
una matokeo ya aina tatu, kushinda, kushindwa na kutoa sare kama
ilivyotokea kwa Simba, hivyo hakuna haja ya kufanya vurugu.
Lakini
inaonekana jaziba hii imetokana na matokeo ya mechi iliyopita ambapo
Simba sc walilala dhidi ya Azam fc huku watani wao wa jadi wakishinda
dhidi ya Mgambo Shooting mabao 3-0 na kukaa nafasi ya tatu katika
msimamo.
Kwa
kawaida matokeo ya timu za Simba na Yanga huwa yanaathiriana sana kwa
mashabiki kwani mmoja akishinda anataka na yeye ashinde kwa vyovyote
vile, kumbe hesabu za mpira hazipo hivyo.
Kutokukubali
matokeo katika soka huwa kunaleta migongano na vurugu kama hizo
uwanjani, hivyo lazima mashabiki wa soka wajifunze kuwa watulivu na
kukubaliana na matokeo kwani haijaandikwa kuwa lazima Simba au Yanga
ishinde katika mchezo, kila timu ina haki ya kushinda.
0 comments:
Post a Comment