Na Mwandishi Wetu
Mashabiki
wa Simba na Yanga mjini Songea watamenyana vikali katika michezo
mbalimbali kupitia bonanza maalum la Nani Mtani Jembe lililoandaliwa na
Bia ya Kilimanjaro Premium Lager litakalofanyika uwanja wa Maji Maji
mjini Songea Jumapili wikendi hii.
Mratibu
wa bonanza hilo Amadeus Kalumuna, amesema kuwa michezo mbalimbali
ikiwemo soka bonanza la wachezaji saba kila upande, kuvuta kamba, na pia
mpira wa mezani maarufu kama fussball itapamba bonanza hilo. Burudani
mbalimbali pia zitapamba bonanza hilo zikiwemo burudani ya muziki kutoka
bendi ya Mastaa wa Kusini, kikundi cha sanaa cha Umoja Star au maarufu
kama “Manyoka”, wacheza show wa Chicharito Group pamoja na wasanii
mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa mkoani Ruvuma.
Kalumuna
pia amesema kuwa vilevile kuwa michezo mbalimbali ya kujifurahisha kama
vile kufukuza kuku wa kienyeji, kukimbia na gunia na kupiga penati
ukiwa umefungwa kitambaa usoni itapamba bonanza hilo ambalo ni la kwanza
kufanyika katika mkoa wa Ruvuma kupitia Nani Mtani Jembe. Kampeni hii
ya aina yake inatoa fursa ya kipekee kwa mashabiki hao kujumuika pamoja
na kuburudika na vile vile imeongeza chachu ya ushindani na utani wa
jadi kati ya mashabiki hao huku ikiwapa fursa ya kipekee kuonyesha
mapenzi kwa timu zao.
Bonanza
hilo linalotarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ni mwendelezo wa kampeni ya
Nani Mtani Jembe ambayo ilizinduliwa Oktoba 2 na inafanyika nchi nzima
ikiwashirikisha mashabiki wa timu kongwe za Simba na Yanga. Kupitia
kampeni hiyo, Kilimanjaro Premium Lager inayozidhamini timu za Simba ya
Yanga imetenga kiasi cha shilingi milioni 100 na kisha kuzigawanya kwa
timu hizo ambapo kila timu inazo shilingi milioni 50 ambazo
zinashindaniwa na mashabiki wao.
Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe alisema kuwa mashabikiwa Simba na
Yanga wanatakiwa kushindana kwa kushiriki kwenye kampeni hiyo ili
kuhakikisha kuwa timu mojawapo inapata fedha nyingi zaidi ya timu
nyingine.
Akielezea
namna ya kushiriki, Kavishe alisema kuwa mpaka kila timu imetengewa
shilingi milioni 50 na kuwa mshiriki wa shindano hilo la Nani Mtani
Jembe ambaye ni shabiki wa Simba au Yanga anachotakiwa kufanya ni
kununua bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo kwenye kizibo chake kuna
namba ya kushiriki.
Alisema
baada ya shabiki kununua bia ya Kilimanjaro na kuona namba ya kwenye
kizibo, anachotakiwa kufanya ni kuchukua simu yake ya kiganjani na
kuandika ujumbe mfupi wa maneno akianza na jina la timu anayoshabikia
kisha anaandika namba iliyo kwenye kizibo na kuituma kwenye namba 15440.
Alisema
baada ya shabiki kutuma namba hiyo, atakuwa amepunguza shilingi 1,000
kutoka kwa timu pinzani yaani ikiwa shabiki aliyetuma ujumbe huo ni wa
Simba atakuwa amefanikiwa kupunguza shilingi 1,000 kutoka kwenye fungu
la Yanga na ikiwa shabiki ni wa Yanga pia atakuwa amepunguza shilingi
1,000 kutoka kwa Simba.
Kwa
mujibu wa Kavishe matokeo ya uwiano wa fedha zinavyopungua kutoka Simba
au Yanga yatangazwa kila siku hadi siku ya mwisho wa shindano hilo
Desemba 14, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment