
Salamu za shukrani
Familia
ya Kakore ya Dar es Salaam, tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa watu
mbalimbali waliofanikisha shughuli nzima za mazishi ya ndugu yetu
mpendwa, Mwalimu Jasper Rashid Kakore (71), aliyefariki ghafla asubuhi
ya Jumapili, Oktoba 20 na kuzikwa Jumatano Oktoba 23 mwaka 2013.
Shukrani
ziwafikie wafanyakazi wote wa Kampuni ya Gapco Tanzania, Kika
Contraction, New Habari 2006 Ltd, Wizara ya Fedha (Hazina) na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Ukaguzi Kanda ya Mashariki), Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Pande, Wachungaji,
Wainjilisti na watumishi wa K.K.K.T Usharika wa Mramba.
Pia
wanachama wa Umoja wa Wanamtaa wa Tuna wa Dar es Salaam, Wanachama wa
Umoja wa Wanakijiji wa Chome wa Dar es Salaam, Wafanyakazi wote wa
Hospitali za Gonja, Apolo na Hospitali ya Wilaya ya Same, wafanyakazi na
wanafunzi wa Shule za Sekondari Same na Dindimo.
Kadhalika
tunapenda kuwashukuru Wanakijiji wa Gonja na Wanamtaa wa Vuje pia
mitandao mbalimbali ya kijamii (Blogs) ndugu, jamaa na marafiki.
Tunaelewa
kuwa watu ni wengi waliojitoa kwa ajili yetu hivyo kwa yeyote ambaye
kwa namna moja ama nyingine hatukuweza kumtaja tunaomba radhi ila
tunathamini sana kile ulichokitoa kwa ajili yetu.
Kama
familia hatuna la kuwalipa ila Mungu aliyewapa moyo wa kujitoa ndiye
atakayewarudishia mali na kila mlichotoa kwa ajili yetu.
0 comments:
Post a Comment