“PRESS RELEASE” TAREHE 18. 09. 2013.  
WILAYA YA MBEYA MJINI    - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
 TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 06:30HRS HUKO MWANJELWA BARABARA YA  
MBEYA/IRINGA JIJI NA  MKOA WA MBEYA.  GARI T.387 BMN AINA YA  TOYOTA 
COASTER LIKIENDESHWA NA  DEREVA HANSI S/O HUMPHREY, MIAKA 37, KYUSA, 
MKAZI WA KYELA  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU WESTON S/O HEPA MWALINGO, 
MIAKA 83, MSAFWA,  MKAZI WA AIRPORT NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO 
HAPO.  CHANZO  KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI 
YA  RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE 
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
 DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI 
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA 
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI -   AJALI YA MPANDA PIKIPIKI KUMGONA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
| 
 | 
MNAMO
 TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO MBALIZI BARABARA YA 
TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI  MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI NA 
DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU  REUBEN S/O MWAKALOBO, 
MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE 
PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA 
BAADA YA  TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI TEULE YA  
IFISI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI 
DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI 
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA 
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAI 
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA PIKIPIKI 
AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO 
AJISALIMISHE  MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO
 TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA  SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO KYELA KATI 
WILAYA YA  KYELA  MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA
 LUGANO S/O RICHARD, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KYELA – KATI 
 AKIWA NA BHANGI GRAM 20. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA 
SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA 
POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  
ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME 
CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO
 TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA BAR IITWAYO NURU 
INN ENEO LA MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA.  ALIKAMATWA 
ERICK S/O JAMSON, MIAKA 25, MSAFWA, MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA NOTI BANDIA
 MOJA YA TSHS 10,000/= YENYE NAMBA – DT 2937833. MBINU NI KUTAKA KUNUNUA
 VINYWAJI KWA KUTUMIA PESA HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE 
MAHAKAMANI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA 
POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII  HASA KATIKA MAENEO YA  
KIBIASHARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA  PESA ILI KUJIEPUSHA NA WATU 
WANAOTUMIA PESA BANDIA . AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU 
YA MTANDAO WA  WATU WANAOMILIKI PESA BANDIA  AZITOE KATIKA MAMLAKA 
HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed by:
                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


0 comments:
Post a Comment