Na Baraka Mpenja, Mbeya
MZUNGUKO
wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara unatarajiwa kuendelea kushika
kasi hapo kesho kwa timu zote 14 kushuka dimbani katika viwanja tofauti
nchini.
Wekundu
wa Msimbazi Simba watakuwa uwanja wao wa nyumbani wa Taifa jijini Dar
es salaam baada ya mechi mbili za Ugenini dhidi ya wakata miwa wa
mashamba ya Manungu Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sukari.
Mechi
hiyo imevuta hisia za mashabiki kutokana na ugumu wa wana TamTam ambao
msimu uliopita walivuta sharubu za Simba na kuwatuliaza tuli.
Mabingwa
watetezi wa ligi hiyo, klabu ya Yanga ya Dar es salaam kwa mara ya
kwanza wanatoka ugenini na kesho wana kibarua kizito mbele ya timu mpya
ya Mbeya City ya jijini hapa katika uwanja wa Sokoine.
Kwa
upande wa wagosi wa kaya, Coastal Union wamerejea kwao CCM Mkwakwani
jijini Tanga na hapo kesho wanawakaribisha wachovu wa ligi hiyo,
Tanzania Prisons ambao kwa Sasa wapo mkiani katika msimamo.
Charlse
Mkwasa na Ruvu Shooting yake watakuwa katika uwanja wao wa Mabatini
mkaoni Pwani kukabiliana na Mgambo JKT, huku tambo zikitawala kwa kila
timu kuibuka kidedea katika mchezo huo.
Dimba
la Sh. Amri Abeid Kaluta jijini Arusha litahimili daluga za wenyeji JKT
Oljoro dhidi ya maafande wenzao kutoka Tabora, Rhino Rangers.
Wauza
mitumba wa Ashanti United watakuwa na kibarua katika uwanja wa Azam
Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam kuwakabili vinara wa ligi
hiyo, JKT Ruvu ambao wametamba kuwa hakuna atakayewatoa kileleni kwa
sasa.

Macho
ya mashabiki wengi wa Soko yatakuwa katika mechi za vigogo wa Soka la
Tanzania, Simba na Yanga pamoja na Azam fc kwani ni ukweli kuwa timu
hizi zinavuta hisia za mashabiki wengi kila kona ya Tanzania.

Kwa
Mbeya, homa ya pambano la kesho inazidi kupanda huku kila kona hadithi
ikiwa ni mechi hiyo ambayo inatarajiwa kushuhudiwa na maelfu ya
mashabiki wa soka kwa kiingilio cha Tsh. 5,000/=.
Chama
cha soka mkoani Mbeya, MREFA kimesema Maandalizi ya mechi hiyo
yamekamilika kuanzia masuala ya uuzaji wa tiketi na ulinzi kwa
kushirikiana na jeshi la polisi.
0 comments:
Post a Comment