Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Raia Cameroon, Samuel Eto’o amefichua siri kuwa alikuwa anamchukia sana kocha wake Jose Mourinho kabla ya kufanya kazi pamoja Inter Milani.
Mwaka
2009/2010, Mourinho aliipandisha sana Inter, huku Eto’o akifanya kazi
kubwa sana baada ya kusajiliwana kurithi mikoba ya Ibra Cadabra, Zlatan
Ibrahimovic .

Marafiki wamekutana: Mshambuliaji mpya wa Chelsea, Samuel Eto’o amefurahi kufanya kazi kwa mara nyigine na kocha Jose Mourinho
“Kabla
ya kukutana Inter, hatukujuana hata kidogo, kwahiyo mahusiano yetu
yalikuwa mabaya sana, Eto’o ameliambia gazetila The Sun. “Ilifika wakati
nikasema sitakuja kucheza klabu ambayo kocha Jose anafundisha”.
“Lakini
Mungu anajua zaidi. Alitaka kunionesha kuwa sikuwa sahihi na leo hii
Jose ni rafiki yangu mkubwa. Sasa ni kocha wangu tena”. Alisema
Mcameroon huyo mwenye mafanikio makubwa katika maisha yake ya soka.
Eto’o
alijiunga na Chelsea dakika za mwisho za dirisha la usajili, majira ya
kiangazi kwa ada ya pauni milioni 7 akitokea Anzhi Makhachkala baada
ya Mourinho kushindwa kumshawishi Wayne Mark Rooney.

Dole mzazi!: Hatimaye Jose Mourinho amepata mshambuliaji aliyekuwa anamhitaji

Mahusiano ya nguvu? Wawili hawa waliungana pamoja hata huko Italia na kuleta mafanikio makubwa Inter Milan

Mafanikio
makubwa: Inter walishinda kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya na
makombe mawili ya ligi kuu kwa mwaka 2009/2010 wakati Mourinho na
Eto’o wakiwa pale
0 comments:
Post a Comment