ANA ‘wazimu’ wa magari. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu ‘Young Don’ Mrisho Khalfan Ngassa, baada ya kutoa Sh. Milioni 21 kununua gari mpya aina ya Peugeot.
Sasa Ngassa anakuwa na gari 10, kati ya hizo kuna mbili alizowapa wazazi wake, baba na mama yake moja ya familia na tatu za kibiashara.
![]() |
Mkoko mpya wa Young Don; Gari jipya la Mrisho Khalfan Ngassa |
![]() |
Ngassa katika gari lake jipya |
Kwa sasa, Ngassa ameiambia BIN ZUBEIRY atakuwa anatumia zaidi ‘mkoko’ wake mpya badala ya ile Nissan ambayo amekuwa akionekana nayo siku za karibuni.
Wakati fulani, alionekana na Prado kwenye mazoezi ya Yanga na kuhusu gari hilo, Ngassa anasema; “Halikuwa gari langu lile, kuna mjomba wangu alichukua gari langu akaniachia lile la kwake,”alisema.
Kwa sasa Ngassa yuko Mwanza alipokwenda kuhudhuria mazishi ya bibi yake mzaa baba, Bi Joha aliyefariki dunia mapema wiki hii.
![]() |
Magari ya Ngassa yamepagana nyumbani kwake |
![]() |
Ni gari kali |
Mtoto huyo wa kiungo wa zamani wa Simba SC, Khalfan Ngassa ‘Babu’ anatarajiwa kupanda ndege leo mjini Mwanza kwenda Mbeya kuungana na timu yake, Yanga SC ambayo ipo huko kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji Mbeya City kesho.
Hata hivyo, Ngassa kwa sasa hachezi kutokana na kuwa bado anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi sita na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusaini timu mbili, Simba na Yanga SC. Tayari amekosa mechi tatu.
![]() |
Ngassa kwenye mazishi ya bibi yake |
0 comments:
Post a Comment