Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi
katika uzinduzi wa mradi wa vibanda vya biashara katika uwanja wa
Kambarage huku akishuhudiwa na Balozi wa China nchini Dr.Lu Youqinq.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka kwa baiskeli kutoka
Uwanja wa Kambarage kuelekea uwanja wa Shycom kwenye mkutano wa hadhara.
Balozi
wa China nchini Dk.Lu Youqinq akiwapungia wananchi wakati akielekea
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya
Shycom,Shinyanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Balozi wa
China nchini wakiwasubiri wenzao tayari kuelekea kwenye uwanja wa Shycom
ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Kutoka kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Balozi wa China nchini na Mbunge
wa Shinyanga mjini Steven Masele wakiendesha baiskeli kuelekea kwenye
uwanja wa Shycom ambapo mkutano mkubwa na wa kihistoria ulifanyika leo
tarehe 13 Septemba 2013.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiingia kwenye uwanja wa Shycom
na baiskeli tayari kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto),Balozi wa China
nchini Dk. Lu Youqinq na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,
Balozi wa China alipata fursa ya kuelezea kwa wananchi wa Shinyanga
namna uwekezaji utaweza kuunufaisha mkoa huo ambapo viwanda vya nguo,
kusindika mafuta, asali na bidhaa zitokanazo na mifugo vinategemewa
kujengwa katika mkuo huo na kutoa nafasi kwa ajira ,kuinua uchumi ,elimu
na kuondoa kabisa umasikini.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shinyanga
mjini katika mkutano wa hadhara uliofanyiaka kwenye uwanja wa Shycom
mkoani Shinyanga.
Mbunge
wa Shinyanga mjini Ndugu Steven Masele akihutubia wakazi wa Shinyanga
mjini na kuwaambia yeye anachofanya ni kutekeleza ilani ya uchaguzi ya
CCM na kwake maendeleo kwa wana Shinyanga ndio kitu cha msingi.
MNEC
wa Wilaya ya Shinyanga mjini Ndugu Gasper Kileo akihutubia wakazi wa
Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya
Shycom,mkoani Shinyanga leo.
Mbunge
wa Viti maalum kupitia UWT Shinyanga Ndugu Lucy Mayenga akiwahutubia
wakazi wa Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu alikuwa
anahitimisha ziara yake mkoani hapo.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Ndugu Azah Hilal Hamad akiwasalimu
wakazi wa Shinyanga mjini wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM Taifa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shinyanga
mjini ambapo aliwaasa wananchi waepuke ‘makanjanja wa siasa’ na badala
yake washirikiane na viongozi wao katika kuleta maendeleo.
Umati wa watu uliofurika wakati wa mkutano wa mwisho wa hadhara wa
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Shycom.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akisoma vijiji
vitavyofaidika na mradi wa umeme vijijini kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom leo tarehe 13 Septemba 2013.
Mbunge wa Kishapu akiruka kwa furaha baada ya kusikia vijiji vya wilaya yake vitafaidika na mradi wa umeme wa vijiji.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu pikipiki mpya
watakazopewa makatibu kata wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Katibu
Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye wakiondoka uwanja wa Shycom baada ya kumaliza mkutano wenye
mafanikio makubwa kwa wakazi wa Shinyanga kwani walipata fursa ya
kutambua namna mkoa wao utakavyobadilika ndani ya miaka 10 ijayo kwani
wawekezaji wa kutoka China wameanza kuwekeza viwanda amabavyo vitatoa
ajira za kutosha, kuinua uchumi kwa wakulima na pia kutoa elimu ya
kilimo na teknolojia.
0 comments:
Post a Comment