Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail
KOCHA
Arsene Wenger amesema hatima yake kuinoa Asernal akiwa kocha mkuu
itaamuliwa na kufanikiwa au kushindwa kupata mafanikio katika kikosi
chake anachokijenga kwa sasa baada ya kumsajili na Mesut Ozil na kuvunja
rekodi ya klabu yake.
Mkataba
wa Wenger unamalizika mwezi juni mwakani amesema aliamua kumsajili
kiungo huyo Mjerumani kwa ada ya pauni milioni 42.5 akiwa na lengo la
klabu yake kuwekeza zaidi na kupata mafanikio makubwa.
Alipoulizwa
jana kama amefungua mazungumzo kuhusu mkataba mpya, kocha huyo mwenye
miaka 63 alisema: “Hatuna haraka. Tuko mwezi wa tisa na mkataba
unamalizika juni mwakani. Kuna muda mrefu kuzungumza hilo. Hukuna haja
ya kupanga”.

Hatima ya baadaye haijulikani: Arsene Wenger akiwa na nyota wake mpya Mesut Ozil hapo jana katka mkutano na waandishi wa habari

Mazoezini Colney: Arsene Wenger, Mesut Ozil, Per Mertesacker na kocha msaidizi Steve Bould

Ukame wa makombe: Arsenal kwa mara ya mwisho walinyanyua kombe la FA 2005 katika dimba la Millennium
“Nimekuwa
nikisema mara nyingi kuwa nataka kufanya vizuri na timu hii na mwishoni
nitakaa chini na kutafakari ni kwa namna gani nimefanikiwa. Hiyo
itatosha kwangu kuamua kama nitabaki au la”. Alisema Wenger.
“Moja kati ya mambo makubwa ya kocha ni kuona namna gani amefanikiwa akiwa na timu”
Ozil
anaamni anaweza kumaliza ukame wa miaka nane kwa Asernal bila kutwaa
kikombe na anaamini kikosi chake kinaweza kushinda msimu huu wa ligi kuu
soka nchini England.
Baada ya kuondoka Real Madrid, Ozil amesisitiza kuwa ujio wake London kaskazini sio kushuka kwake.
“Sijakata tamaa. Nipo Arsenal sasa, ni moja kati ya klabu kubwa duniani”
“Kiukweli
nilikuwa na wakati mzuri Madrid. Nimewapoteza rafiki zangu na muda
mzuri pale. Sasa nipo ligi ngumu zaidi duniani na natakiwa
kuwahakikishia kuwa nitaendelea kukua zaidi. Na ndio maana nipo katika
klabu sahihi”. Alisema Ozil.

Jembe jipya: Arsene Wenger alivunja benki ya Arsenal na rekodi ya klabu katika usajili wa Mesut Ozil kutoka Real Madrid
0 comments:
Post a Comment