Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
JITIHADA za Romelu Lukaku kuendelea kubakia Chelsea chini ya kocha Jose Mourinho baada ya kucheza kwa mkopo kwa muda mrefu katika klabu ya West Brom, sasa janga limemkuta tena baada ya kocha wake kumtoa tena kwa mkopo wa muda mrefu klabu ya Everton.
Japokuwa amekaa kwa wiki kadhaa msimu huu katika kikosi cha Chelsea, Lukaku amecheza mechi tatu akitoka benchi na mara ya mwisho alicheza katika fainali ya Super Cup na kukosa penati iliyowapa ubingwa Bayern Munich na sasa ametupwa kwa mkopo wa muda mrefu katika dimba la Goodison .

Roberto Martinez amefanikiwa kuinasa saini ya mchezaji huyo licha ya kukata tamaa na pamoja na kutakiwa pia na West Brom ambako mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20alicheza kwa mkopo msimu uliopita- akifunga mabao 17 katika Ligi Kuu.
0 comments:
Post a Comment