Sunday, August 18, 2013

1Baadhi ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika mazoezi mepesi wakati wa safari ya kuelekea katika jiji la Windhoek nchini Namibia.
2Baadhi ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika picha pamoja na Askari wa Kikosi maalumu katika Jeshi la Polisi la Namibia
3Baadhi ya Wanamichezo wanaounda timu ya Polisi wakiwa katika picha katika moja ya miji katika nchi ya Namibia.
Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi-Windhoek Namibia.
Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi,Windhoek Namibia.
Hatimaye timu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Michezo ya Nane ya Umoja wa wakuu wa majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) nchini Namibia imefika salama na imeanza mazoezi mepesi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza jumatatu tarehe 19 mwezi Agosti mwaka huu.
Timu hiyo ambayo ni tishio katika michezo hiyo kutokana na historia yake ya ushindi katika mashindano yaliyotangulia imekuwa kivutio kila inapopita huku kila mmoja akitaka kusalimiana nayo.
Timu hiyo inaundwa na  wanamichezo 67 ambao wanacheza Mpira wa miguu wanaume, Mpira wa pete Wanawake, Riadha wanaumwe na wanawake na mchezo wa Vishale (Dats).
Michezo hiyo itashirikisha Nchi kumi na nne (14) katika michezo mbalimbali na lengo la michezo hiyo ni kujenga ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SARPCCO katika kukabiliana na uhalifu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video