Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
MABINGWA watetezi wa taji la ligi kuu nchini England, Mashetani Wekundu, Manchester United, wametoa kipondo cha mbwa mwizi kwa klabu ya Swensea City cha mabao 4-1.
Wayne Rooney aliingia kipindi cha pili, lakini ni Robin van Persie na Danny Welbeck ambao wamempa mwanzo mzuri zaidi kocha wao David Moyes katika maisha yake klabuni Manchester United.
ARV aliandika bao la kwanza katika dakika ya 34, dakika ya 36 Welbeck aliandika bao la tatu, katika dakika ya 72 ARV aliandika kimiani bao la tatu akipokea pasi nzuri kutoka kwa Wayne Mark Rooney.
Na sherehe ya mabao ilihitimishwa na Welbeck katika dakika 90 akipokea pasi murua kutoka kwa Rooney ambaye ni gumzo kubwa katika usajili wa majira haya ya kiangazi.
Swansea walipata bao la kuwadanganyishia mashabiki wao kuwa walikaza lakini ndio basi tena katika dakika 82 kupitia kwa Bony Wilfried akipokea pasi nzuri kutoka kwa Pablo Hernande.


Kikosi cha Swansea leo: (4-5-1) Vorm 6; Rangel 6, Flores 6, Williams 5, Davies 6; Britton 6 (BOny 45mins 6),Canas 5 (ki 76mins 6), Shelvey 7, Dyer 6, Routledge 6 (Hernandez 45mins 6); Michu 6.
Kikosi cha Manchester United leo : (4-4-2) De Gea 6; Jones 6, Ferdinand 6, Vidic 6, Evra 6; Valencia 6, Carrick 7, Cleverley 7, Giggs 6 (Rooney 61mins 6); Welbeck 8, Van Persie (Anderson 86) 8.



0 comments:
Post a Comment