MARIA DAUDI akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na wasamaria wema nje ya ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, lengo lake lilikuwa kumtaka waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Dkk. Shukuru Kawambwa atoke ili kumueleza shida yake, ambapo nyumba yake ilivunjwa kupisha ujenzi wa wa chuo cha Afya cha muhimbili (MUHANS) huko Kibamba –Mlonganzilo,
MARIA akigalagala chini huku Msamalia mwema akijali kusaidia kumuinua
MMOJA wa wananchi hao akionesha moja ya nakala walizokabidhiwa ili kupatiwa malipo yao.
MMOJA wa watu wa kundi hilo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
Lakini hakutaka jina lake litajwe , ”Waziri ameamua kutukimbia wakati anajua wazi kuwa tumekuja hapa ili atutatuliye kero zetu lakini yeye anaamua kutokea mlango wa nyuma hivi kweli tunajenga taifa la namna gani kama waziri mwenye dhamana unaogopa wananchi wako kuwapa ukweli”. Alisikika akiseme
Mtu huyo alidai mwezi wa saba mwaka jana walilazimishwa kuvunjiwa nyumba zao bila kupewa taarifa mapema hatua iliyowafanya kwenda kwa mkuu wa mkoa ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lao, lakini mpaka hii leo bado hawajapatiwa maelezo ya kueleweka zaidi ya kuzungushwa kila kukicha,
“Ndugu mwandishi sisi kama unavyotuona tuko hapa toka asubuhi , kwanza tuliambiwa twende wizarani tulipofika huko tukaambiwa waziri hayupo ameenda katika mkutano huko viwanja vya Gymkana na ndipo tukaamua kuja kumuona, lakini mpaka sasa hatumuoni huyo waziri”. alisema mtu huyo.

0 comments:
Post a Comment